Wahamiaji takriban 30 wa Afrika wauawa katika mashambulizi ya anga ya Marekani kwenye kituo cha kizuizi nchini Yemen

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 29, 2025

Picha hii ya iliyopigwa kutoka kwenye video ikionyesha waokoaji wakisaidia kumtoa mtu kutoka kwenye vifusi katika kituo cha kizuizi jimboni Saada, Yemen, Aprili 28, 2025. (Houthi Media Center/Handout via Xinhua)

Picha hii kutoka kwenye video ikionyesha waokoaji wakisaidia kumtoa mtu kutoka kwenye vifusi katika kituo cha kizuizi jimboni Saada, Yemen, Aprili 28, 2025. (Picha/CFP)

SANAA - Waasi Wahouthi, ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya kaskazini mwa Yemen, wamesema mashambulizi ya anga ya Marekani uliofanywa mapema jana Jumatatu kwenye kituo cha kizuizi katika jimbo la kaskazini la Saada yameua wahamiaji takriban 30 wa Afrika na wengine 50 kujeruhiwa katika makadirio ya awali.

Televisheni ya al-Masirah inayoeendeshwa na wanamgambo hao Wahouthi imeripoti kwamba miili 30 ilikuwa imetolewa kwenye vifusi huku timu za uokoaji zikiendelea kutafuta manusura wanaowezekana kuwa hai.

Chaneli hiyo ya televisheni imeongeza kuwa majeruhi wengine 50, ambao pia ni wahamiaji haramu wa Afrika, wamepelekwa hospitalini. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha