Chuo Kikuu cha Lugha ya Kichina cha Misri chaadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa

(CRI Online) April 29, 2025

Mamia ya wanafunzi na wapenzi wa lugha ya Kichina walikusanyika juzi Jumapili katika Chuo Kikuu cha Lugha ya Kichina cha Misri (ECU) mjini Cairo kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa.

Akihutubia ufunguzi wa hafla hiyo Konsuli Mkuu wa Ubalozi wa China nchini humo Lu Chunsheng amesema lugha ya Kichina ni chombo kinachobeba mawasiliano, maelewano na heshima na kwamba kujifunza Kichina kunaakisi nguvu kupitia uwazi na uhimilivu, na kujenga madaraja badala ya vizuizi.

Ofisa huyo pia amebainisha kuwa kwa sasa Misri imefungua idara 32 za lugha ya kichina katika vyuo vikuu, taasisi tatu za Confucius na madarasa mawili ya Confucius.

Mkuu wa chuo kikuu cha ECU Rasha El-Kholy amesema katika miaka ya hivi karibuni ushirikiano kati ya Misri na China kwenye sekta ya sayansi na elimu umeongezeka, zikiwemo fursa za kujifunza nchini China, miradi ya mafunzo kwa walimu na shughuli za kambi za majira ya joto kwa wanafunzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha