

Lugha Nyingine
OPCW lahimiza uwepo wa sheria kali za silaha za kemikali barani Afrika
Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali Duniani (OPCW) limezitaka nchi za Afrika kuimarisha utekelezaji wa Mkataba wa Silaha za Kemikali (CWC).
Wito huo umetolewa kwenye mkutano wa siku mbili wa kikanda kuhusu silaha za kemikali ulioanza Jumatatu mjini Windhoek, Namibia.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa OPCW Bibi Odette Melono amesisitiza kuwa utekelezaji thabiti wa sheria ni muhimu katika kulinda kanuni ya kimataifa ya kuzuia silaha za kemikali na kujitokeza kwake tena.
Bibi Melono amesema kupitishwa kwa mkataba wa CWC na nchi 193, kunaonesha Afrika iko nyuma, huku akiongeza kuwa ni asilimia 48 tu ya nchi wanachama kutoka Afrika ndiyo zimepitisha sheria husika za kitaifa, na bado kuna nchi 27 ambazo hazina sheria au zina nusu sheria zinazosimamia utekelezaji wa wajibu wao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma