

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atembelea Benki ya Maendeleo Mapya
Rais wa China Xi Jinping akitembelea Benki ya Maendeleo Mapya na kukutana na Dilma Rousseff, mkuu wa benki hiyo, mjini Shanghai, mashariki mwa China, Aprili 29, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
SHANGHAI - Rais wa China Xi Jinping jana Jumanne alitembelea Benki ya Maendeleo Mapya mjini Shanghai na kukutana na Dilma Rousseff, mkuu wa benki hiyo, ambapo amempongeza Rousseff kwa kuchaguliwa tena kuwa mkuu wa Benki ya Maendeleo Mapya, na amesema kuwa benki hiyo ni taasisi ya kwanza duniani ya maendeleo ya pande nyingi iliyoanzishwa na kuongozwa na nchi zenye masoko yanayoibukia na zinazoendelea.
Rousseff aliwaongoza manaibu wakuu wanne wa benki hiyo na wafanyakazi wengine kumkaribisha Rais Xi alipofika.
Rais Xi amesema benki hiyo ni "juhudi anzilishi za mfano wa kushirikisha na kujiimarisha kwa Nchi za Kusini," na inaendana na wimbi la historia la kuufanyia mageuzi na kuuboresha usimamizi wa Dunia.
"Benki ya Maendeleo Mapya imeibuka kuwa nguvu inayoinuka katika mfumo wa mambo ya fedha wa kimataifa na mfano unaong'aa wa ushirikiano wa Nchi za Kusini," amesema.
Amesisitiza kuwa ushirikiano mpana wa BRICS umeingia katika hatua ya maendeleo ya sifa bora ya juu, na benki hiyo inatakiwa kuanzisha muongo wake wa pili wa dhahabu wa maendeleo ya sifa bora.
Rais Xi ametumai benki hiyo kuzingatia mahitaji ya maendeleo ya Nchi za Kusini, na kutoa ufadhili zaidi kwa miundombinu ulio wa kiwango cha juu, bei ya chini na endelevu.
"Benki inahitaji kuboresha usimamizi na uendeshaji wake, kutekeleza miradi zaidi ya mambo ya fedha kwa ajili ya teknolojia na maendeleo ya kijani, na kusaidia nchi zinazoendelea kuziba pengo la kidijitali na kuharakisha mageuzi ya kijani na yenye kutoa kaboni chache," Rais Xi amesema.
Amesema, katika majadiliano juu ya mageuzi ya usanifu wa mfumo wa mambo ya fedha wa kimataifa, benki hiyo inapaswa kupaza sauti ya Nchi za Kusini, kulinda haki na maslahi halali ya Nchi za Kusini, na kuunga mkono Nchi za Kusini katika kutafuta ujenzi wa mambo ya kisasa.
Amesema kuwa China ikiwa nchi mwenyeji wa benki hiyo, siku zote inaunga mkono shughuli na maendeleo ya Benki ya Maendeleo Mapya. China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kimradi na benki hiyo na kujikita katika maendeleo ya kijani, kivumbuzi na endelevu ili kupata matokeo zaidi.
Kwa upande wake Rousseff ametoa shukrani zake kwa China kwa uungaji wake mkono wa muda mrefu kwa ukuaji na upanuzi wa Benki ya Maendeleo Mapya.
Amesema kuwa chini ya uongozi wa Rais Xi, China imepata mafanikio ya maendeleo yasiyo ya kawaida na kuonesha umuhimu wake katika kuendeleza usimamizi wa Dunia, na ina hakika kufikia matarajio yake ya ustawishaji mkubwa wa taifa la China.
Ameongeza kuwa, licha ya hali yenye msukosuko katika dunia ya hivi sasa, serikali ya China imesimama kidete kulinda maslahi ya Nchi za Kusini, kuunga mkono ushirikiano wa pande nyingi, kutetea haki na usawa wa kimataifa, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, ikiweka mfano kwa jumuiya ya kimataifa.
Rais wa China Xi Jinping akitembelea Benki ya Maendeleo Mapya na kukutana na Dilma Rousseff, mkuu wa benki hiyo mjini Shanghai, mashariki mwa China, Aprili 29, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
Rais wa China Xi Jinping akitembelea Benki ya Maendeleo Mapya na kukutana na Dilma Rousseff, mkuu wa benki hiyo mjini Shanghai, mashariki mwa China, Aprili 29, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma