

Lugha Nyingine
Reli ya mwendokasi ya Jakarta-Bandung, Indonesia yasafirisha abiria milioni 9 tangu kuzinduliwa
![]() |
Abiria wanaowasili wakionekana katika picha kwenye jukwaa la Stesheni ya Reli ya Halim mjini Jakarta, Indonesia, Aprili 24, 2025. (Xinhua/Xu Qin) |
JAKARTA - Reli ya Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung nchini Indonesia, inayojulikana na wenyeji kwa jina la Whoosh, imesafirisha abiria milioni 9 kufikia Jumapili ya wiki iliyopita tangu kuzinduliwa kwake Oktoba 17, mwaka 2023, PT Kereta Cepat Indonesia-China (KCIC), kampuni ya ubia kati ya kampuni za Indonesia na China iliyojenga na kuendesha reli hiyo imetangaza juzi Jumatatu.
KCIC pia imesema kuwa hadi kufikia Jumapili, Whoosh ilikuwa imeendesha jumla ya safari za treni 26,168, zikifika kilomita zaidi ya milioni 4.11.
Kama njia kuu ya usafiri kati ya Jakarta na Bandung, Whoosh imepata umaarufu, ikitoa uzoefu wa usafiri ulio salama, wa kijani, wenye ufanisi na mzuri. Kwa sasa, kampuni hiyo inaendesha huduma za treni 62 kwa siku, huku idadi ya juu zaidi ya abiria kwa siku moja ikifikia 24,350.
Wakati wa likizo ya hivi karibuni ya Eid al-Fitr mapema mwezi huu, idadi ya abiria iliongezeka sana ambapo KCIC imeeleza kuwa ilirekodi abiria 341,100 waliokuwa wakisafiri kwa Whoosh wakati wa likizo. Imesema, kiwango cha abiria kwa siku kilikuwa kati ya 16,500 na 23,500, na idadi ya wasafiri ilifikia wasafiri 23,500 katika Aprili 6, idadi ambayo ni cha juu zaidi.
Ikiwa imejengwa na kuendeshwa kwa pamoja na China na Indonesia, reli hiyo ya mwendo kasi ya Whoosh ina urefu wa kilomita 142.3 na inafanya kazi kwa kasi ya juu zaidi ya kilomita 350 kwa saa, ikipunguza muda wa usafiri kati ya Jakarta na Bandung kutoka zaidi ya saa tatu hadi dakika 46.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma