Naibu Waziri Mkuu: DRC kuzidisha zaidi ushirikiano na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 30, 2025

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jacquemain Shabani  akishiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa majengo mapya ya Ubalozi wa China  huko Kinshasa, mji mkuu wa DRC, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Shi Yu)

KINSHASA - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itazidisha ushirikiano na China katika sekta mbalimbali, amesema Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa nchi hiyo Jacquemain Shabani juzi Jumatatu wakati akishiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa majengo mapya ya Ubalozi wa China mjini Kinshasa.

Shabani amesema DRC na China zitachukua uzinduzi wa jengo jipya hilo la ubalozi kuwa fursa ya kuzidisha zaidi ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuhimiza ujenzi wa miradi ya kijamii na miundombinu ili kunufaisha wananchi.

Balozi wa China nchini DRC Zhao Bin amesema, urafiki wa kina kati ya watu wa nchi hizo mbili ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya siku hadi siku ya uhusiano wa pande mbili, China itaendelea kuandaa "Wiki ya Filamu ya China" na shughuli nyingine za kitamaduni, na kualika marafiki zaidi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutembelea majengo mapya ya mambo ya kidiplomasia ili kuwawezesha kuijua zaidi China. 

Balozi wa China katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Zhao Bin  akishiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa majengo mapya ya Ubalozi wa China  huko Kinshasa, mji mkuu wa DRC, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Shi Yu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha