

Lugha Nyingine
Dunia inataka haki, haitaki Umwamba | Maoni ya People's Daily Online kuhusu Utozaji Kiholela wa Kodi wa Marekani 1
Hivi karibuni, serikali ya Marekani, kwa kile kinachoitwa "kutozana kodi kwa usawa", imefika hadi kutoza kodi ya juu kwa nchi na maeneo zaidi ya 180 kote duniani. Hali hii ya ajabu ambayo hata pengwini na sili wamekuwa walengwa wa kutozwa kodi inatokana na mantiki ya umwamba wa upande mmoja ya "wenye nguvu kuwadhulu wanyonge". Serikali ya Marekani inashikilia kwa ukaidi kwenda kinyume cha wimbi la historia, inaumiza wengine na kujiumiza yenyewe!
Kitendo cha umwamba cha serikali ya Marekani kinatafuta ubinafsi wake yenyewe, na inazuia haki ya kujiendeleza ya nchi mbalimbali duniani, haswa nchi dhaifu zaidi. Kutoza kodi ya juu zaidi ya uwezo wa nchi ndogo iliyo na muundo mmoja wa kiuchumi, kwa kweli ni kutumia umwamba kwa kupindua utaratibu wa biashara wa pande nyingi, na kujipatia maslahi ya kimataifa.
Kitendo hicho cha umwamba cha serikali ya Marekani si kama tu kinaumiza watu wa nchi nyingine, bali pia kinaleta matatizo makubwa kwa watu wa Marekani. Utozaji wa kodi ya juu utapandisha bei za bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, na mfumuko wa bei unaosababishwa na hali hiyo utaongeza kwa kiasi kikubwa gharama za maisha kwa familia za kawaida za Marekani; utozaji wa kodi ya juu unaweza kusababisha Wamarekani wapatao milioni 2 kupoteza ajira zao, na kila familia ya Marekani itakabiliwa na hasara ya mapato ya angalau dola za Kimarekani 5,000; hatari ya kudorora kwa uchumi itaongezeka, mkopo wa dola ya Marekani utaathiriwa, na mali za dola ya Marekani zitauzwa kwa kiwango kikubwa; hali ya kutokuwa na uhakika kwenye soko la kimataifa itaongezeka, ambayo haitasaidia kampuni za Marekani kupanua soko lake nje, na itaathiri biashara ya nje ya Marekani. Na zimekuwa na sauti zaidi za upingaji nchini Marekani. Aprili 23, majimbo 12 ya Marekani yaliunda muungano wa kuishtaki serikali kuu ya Marekani kwa pamoja, yakiishutumu sera yake ya utozaji kodi kukiuka sheria.
Historia kwa muda mrefu imekuwa ikithibitisha kwamba vita vya biashara na vita vya utozaji kodi vitaumiza tu pande zote mbili. Katika miaka ya 1930, Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Smoot-Hawley ilisababisha Mdororo Mkuu wa Uchumi duniani (Great Depression); hivi leo, serikali ya Marekani inarudia makosa yale yale na yanaelekea kuirudia yenyewe. Maabara ya Bajeti ya Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani inakadiria kuwa utekelezaji wa hatua zote za utozaji kodi mwaka 2025 utapunguza kasi ya ongezeko halisi la Pato la Taifa la Marekani kwa asilimia 1.1 mwaka huo, na kasi ya ongezeko la Pato la Taifa katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu itashuka kwa asilimia 0.6.
Dunia inataka haki, na haitaki umwamba. Katika mazingira ya hivi sasa ya mtandao wa uchumi wa dunia, uchumi wa nchi mbalimbali unategemeana, na kubadilikabadilika kiuchumi katika nchi yoyote kunaweza kuleta athari pia kwa nchi nyingine. Kwenye mkutano wa mwaka wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bidhaa ya WTO uliofanyika hivi karibuni, ufuatiliaji mkubwa wa China kuhusu "hatua za serikali ya Marekani za kutoza ovyo kodi" uliitikiwa na nchi 46. Tunaamini kwamba idadi kubwa ya nchi zinazoamini haki na usawa zitafanya chaguo sahihi kwa maslahi yao zenyewe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma