

Lugha Nyingine
Kenya yawasilisha kwa Umoja wa Mataifa mpango kuhusu tabianchi wenye lengo la kupunguza uchafuzi kwa asilimia 35
Kenya imewasilisha Mpango wake wa Pili wa Taifa (NDCs) kwa Mkataba wa Mfumokazi wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, ukieleza hatua zake za kupunguza utoaji wa hewa chafu na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kuanzia 2031 hadi 2035.
Chini ya Makubaliano ya Paris, nchi mbalimbali zinatakiwa kuwasilisha mipango iliyorekebishwa, au malengo ya kitaifa ya kupunguza hewa za kaboni, kila baada ya miaka mitano.
Kenya ilifikia tarehe yake ya mwisho ya Aprili 30, 2025, na wasilisho lake jipya linalenga kupunguza utoaji wa hewa chafu kwa asilimia 35 ifikapo 2035, sawa na kuondoa tani milioni 75.25 za hewa ya ukaa kutoka hewani.
Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu wa Kenya Bibi Deborah Barasa, amesema Kenya inatazamia kuwa na jamii inayostahimili tabianchi ambapo maisha, jamii, sekta za kijamii na kiuchumi, miundombinu, na mifumo ya ikolojia, itastawi licha ya athari za sasa na zinazotarajiwa za mabadiliko ya tabia nchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma