Rais Xi Jinping ahimiza vijana kuchangia kwenye ujenzi wa mambo ya kisasa wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 04, 2025

BEIJING - Rais Xi Jinping kwenye barua ya majibu kwa kundi la walimu wa kujitolea wanaofanya kazi katika shule ya mpakani katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China ametoa wito kwa vijana wa China kujitolea kwa ujenzi wa mambo ya kisasa za nchi kwa kutumikia mahali ambako taifa linawahitaji zaidi.

Katika kuadhimisha Siku ya Vijana ya China ambayo ni leo Mei 4, Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa salamu za sherehe kwa vijana kote nchini China na kueleza matarajio makubwa kwa mchango wao katika barua hiyo.

Amewapongeza wafanyakazi hao wa kujitolea ambao wanatumikia katika shule ya msingi katika Kitongoji cha Karajol, Mji wa Artux, Eneo linalojiendesha la Kabila la Wakirgiz la Kizilsu. Shule hiyo ya kijiji inapatikana umbali wa kilomita 47 tu kutoka mpaka wa China.

"Mmeitikia wito wa Chama kwa kufundisha katika maeneo ya mpakani ya magharibi, ambapo jitihada zenu si tu zimehimiza elimu ya wenyeji na umoja wa kikabila lakini pia zimechangia ustawi na utulivu katika mpaka," Rais Xi amesema.

Rais Xi amesema kuwa vijana wengi zaidi wamekuwa wakichagua kuhudumu kama watu wa kujitolea katika mikoa ya magharibi na vijijini nchini humo kwa miaka mingi, wakionyesha moyo wao wa kujitolea na hisia ya kuwajibika.

Amehimiza vijana kusimama kidete katika misimamo na mambo yao wanayoyaamini, kujenga uzalendo, kuendeleza ujuzi wa hali ya juu, na kufanya kazi kwa bidii ili kuchangia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Hivi karibuni, wafanyakazi hao wa kujitolea walimwandikia Rais Xi barua kueleza uzoefu wao na kusisitiza kujitolea kwao kuhudumu katika maeneo ya mpakani ya China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha