

Lugha Nyingine
Rais Xi kufanya ziara ya kiserikali nchini Russia, kushiriki kwenye sherehe za Ushindi wa Vita vikubwa vya kulinda nchi Mei 7-10
BEIJING – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema Jumapili iliyopita kuwa, Rais wa China Xi Jinping atafanya ziara ya kiserikali nchini Russia kuanzia Mei 7 hadi 10 na kushiriki kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana Ushindi katika Vita vikubwa vya kulinda nchi mjini Moscow kutokana na mwaliko wa Rais Vladimir Putin wa Shirikisho la Russia.
Msemaji huyo amefahamisha kuwa katika ziara hiyo ijayo ya kiserikali, Rais Xi atakuwa na mazungumzo ya kimkakati na Rais Putin kuhusu uhusiano kati ya China na Russia chini ya mazingira mapya pamoja na masuala makubwa mbalimbali ya kimataifa na kikanda.
"Tunaamini maelewano muhimu ya pamoja kati ya marais hao wawili yatazidisha kuaminiana kisiasa kati ya nchi hizo mbili, kuongeza mambo mapya katika uratibu wa kimkakati, kuhimiza ushirikiano wa kufuata hali halisi katika sekta mbalimbali, kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili, na kuchangia utulivu na nishati chanya zaidi kwa jumuiya ya kimataifa," msemaji huyo amesema.
Msemaji huyo akisema mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa Vita vya Watu wa China vya kupambana na Uvamizi wa Japan, Vita vikubwa vya kulinda nchi na Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti, China na Russia zilikuwa sehemu kuu za mapambano za Asia na Ulaya katika Vita vya Pili vya Dunia, zilijitoa mihanga sana na kutoa mchango mkubwa wa kihistoria kwa ajili ya kupata ushindi katika Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti, na pia kuokoa mustakabali wa binadamu.
“Rais Xi na Rais Putin hapo awali walikubaliana kwamba pande hizo mbili kwa pamoja zitakumbuka historia, kutoa heshima kwa mashujaa waliojitoa mihanga, kujenga mtazamo sahihi wa historia ya Vita vya Pili vya Dunia, kulinda matokeo ya ushindi katika vita na utaratibu wa kimataifa wa baada ya vita, na kulinda haki na usawa wa kimataifa,” msemaji huyo amesema.
Msemaji huyo amesema, katika wakati huu maalum wa kihistoria, Rais Xi kushiriki kwa mwaliko kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana Ushindi katika Vita vikubwa vya kulinda nchi mjini Moscow ni sehemu muhimu ya ziara yake hiyo, na hii pia imeonesha kuwa China na Russia zinaungana mkono kwa kumbukumbu ya kila mmoja ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti.
Msemaji huyo amesema, Mwaka huu pia ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, China na Russia zikiwa nchi wanachama waanzilishi wa Umoja wa Mataifa na wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zinabeba jukumu maalum na muhimu katika kulinda mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma