Kenya yawa mwenyeji wa mkutano kuhimiza mpito kuelekea vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme

(CRI Online) Mei 06, 2025

Kenya Jumatatu imekuwa mwenyeji wa mkutano wa siku mbili wa ngazi ya juu uliolenga kuharakisha matumizi ya suluhu za vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati ya umeme ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuchochea upunguzaji wa hewa ya ukaa.

Tukio hilo la Mkutano wa tatu na Maonesho ya Wadau wa Vyombo vya Usafiri vinavyotumia Umeme limefanyika mjini Nairobi, huku likiwa na wadau zaidi ya 200 walioalikwa kutoka serikalini, mashirika ya maendeleo, na wavumbuzi wa sekta binafsi ili kutafuta fursa za kuongeza magari yanayotumia nishati ya umeme (EVs), miundombinu ya kuchaji magari, na mifumokazi ya sera.

Alex Wachira, katibu mkuu katika Wizara ya Nishati na Petroli ya Kenya, amesema serikali ya nchi hiyo ina nia ya kujenga mazingira wezeshi ndani ya mfumo wa vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme kupitia utoaji wa miundombinu hitajika, ikiwemo vituo vya kuchajia ambavyo vitawawezesha madereva kusafiri kwa urahisi.

Mkuu wa Jumuiya ya Vyombo vya Usafiri vinavyotumia Umeme ya Kenya, Hezbon Mose, amesema kuna takriban vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati ya umeme 9,047 vilivyosajiliwa nchini humo, ambayo vingi ni pikipiki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha