

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Merz kwa kuchaguliwa kuwa Chansela wa Ujerumani
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi jana Jumanne kwa Friedrich Merz kwa kuchaguliwa kuwa Chansela wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.
Rais Xi amesema kuwa China na Ujerumani ni washirika wa kimkakati wa pande zote, na tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 53 iliyopita, nchi hizo mbili zimekuwa zikitendeana kwa kuheshimiana, kuaminiana na kwa usawa.
Rais Xi amesema nchi hizo mbili siku zote zimekuwa zikifuata njia ya ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote, zikikua kuwa washirika wazuri wanaosonga mbele pamoja na kusaidiana kufanikiwa, na kuhimiza maendeleo mazuri na endelevu ya uhusiano wa pande mbili kupitia ushirikiano wa kiwango cha juu.
Rais Xi amesema, “Dunia ya leo umekabiliwa na mabadiliko na misukosuko vinavyoingiliana, huku kukiwa na vizuizi vya uamuzi wa upande mmoja na kujilinda kibiashara,” lakini bado amani, maendeleo, ushirikiano na matokeo yenye manufaa kwa pande zote vinabaki kuwa njia sahihi ya kusonga mbele kwa binadamu na wimbi lisilozuilika la zama tulizonazo.
"Zikiwa nchi zenye uchumi wa pili na wa tatu kwa ukubwa duniani na nchi mbili kubwa zenye ushawishi duniani, China na Ujerumani zinapaswa kufuata mwelekeo wa historia, kushikilia haki na usawa, kuzidisha mawasiliano na kufundishana, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kukabiliana kwa pamoja na dhoruba na tufani, kuongeza ustawi kwa watu wao, na kwa pamoja kuhimiza dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa kiuchumi ulio wa jumuishi.” Rais Xi amesema.
Rais Xi amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ujerumani, na anapenda kufanya juhudi pamoja na Bwana chansela katika kufuata matarajio ya awali ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuzidisha mawasiliano na ushirikiano, na kuanzisha hali mpya ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Ujerumani, ili kuongoza mwelekeo sahihi wa ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, na kwa pamoja kuhimiza amani, utulivu na ustawi wa dunia.
Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu wa China Li Qiang alituma salamu za pongezi kwa Merz kwa kuchaguliwa kuwa Chansela wa Ujerumani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma