Rais wa Mauritius aahidi kuimarisha ushirikiano na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2025

Rais wa Mauritius Dharam Gokhool (kulia) akizungumza na Huang Shifang, Balozi mpya wa China nchini Mauritius,  huko Port Louis, Mauritius, Mei 5, 2025. (Ubalozi wa China nchini Mauritius/kupitia Xinhua)

Rais wa Mauritius Dharam Gokhool (kulia) akizungumza na Huang Shifang, Balozi mpya wa China nchini Mauritius, huko Port Louis, Mauritius, Mei 5, 2025. (Ubalozi wa China nchini Mauritius/kupitia Xinhua)

PORT LOUIS - Rais wa Mauritius Dharam Gokhool ameelezea matumaini yake ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa pande mbili na China katika sekta za uchumi, biashara na utalii, kwa kupitia Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na Mkataba wa Biashara Huria wa Mauritius na China.

Gokhool amesema hayo Jumatatu wiki hii wakati akipokea nyaraka za utambulisho za Huang Shifang, Balozi mpya wa China nchini Mauritius.

Amezungumzia urafiki uliokita mizizi kati ya Mauritius na China, akisisitiza tena kwamba Mauritius inaweka umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wake na China na inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja.

Kwa upande wake, Balozi Huang ameahidi kutimiza wajibu wake kwa uaminifu, kutekeleza matarajio ya pamoja ya wakuu wa nchi hizo mbili, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, na kupanua ushirikiano wa kufuata hali halisi katika sekta mbalimbali, kwa lengo la kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Mauritius.

Balozi Huang aliwasili Mauritius Mei 2.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha