Zaidi ya Faru 100 wauawa nchini Afrika Kusini mwaka huu

(CRI Online) Mei 07, 2025

Zaidi ya Faru 100 wameuawa na majangili nchini Afrika Kusini katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu, wengi wao wakiuliwa ndani ya hifadhi za taifa, ikidhihirisha vita vinavyoendelea ili kulinda moja ya spishi bora zilizo hatarini kutoweka.

Waziri wa Mazingira wa nchini Afrika Kusini Dion George ametoa takwimu hizo jana Jumanne, akisema kuwa miongoni mwa Faru 103 waliouawa kati ya Januari Mosi na Machi 31, 65 wameuliwa katika hifadhi za taifa.

Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi ya Faru duniani, ikikadiriwa kuwa na Faru kati ya 16,000 hadi 18,000, wakiwemo Faru weupe na weusi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha