Ukuaji wa uchumi wa Kenya wapungua hadi asilimia 4.7 mwaka 2024

(CRI Online) Mei 07, 2025

Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Takwimu ya Taifa ya Kenya (KNBS) Bw. Macdonald Obudho amesema, uchumi wa nchi hiyo ulikua kwa asilimia 4.7 mwaka 2024, ukipungua kutoka asilimia 5.7 ya mwaka 2023.

Akiongea na wanahabari mjini Nairobi wakati wa uzinduzi wa Uchunguzi wa Uchumi wa Mwaka 2025, Bw. Obudho amesema ukuaji ulionekana katika sekta nyingi za uchumi huku sekta za kilimo, misitu na uvuvi zikikua kwa asilimia 4.6.

Bw. Obudho amebainisha kuwa sekta ya kilimo imefanya vizuri kwa ujumla mwaka 2024 kutokana na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya nafaka, uzalishaji wa mifugo na ongezeko la uungaji mkono wa serikali kwa sekta hiyo.

Idara hiyo imesema, sekta ya uzalishaji bidhaa viwandani ilikua kwa asilimia 2.8, ikiongezeka kutoka asilimia 2.2 ya mwaka 2023 kutokana na upanuzi wa viwanda vya kilimo unaotokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa sukari.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha