Kampuni ya Reli ya Ethiopia-Djibouti yaahidi kuunda upya mienendo ya biashara na kukuza maendeleo ya kikanda

(CRI Online) Mei 07, 2025

Kampuni Ubia ya Reli ya SGR ya Ethio-Djibouti (EDR) imesisitiza dhamira yake thabiti ya kupanua mchango wa reli iliyojengwa na China kama "mshipa muhimu wa biashara na muunganiko" kati ya nchi hizo mbili, kwa lengo la kuongeza ufanisi wa uchukuzi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kikanda.

Kampuni hiyo ya EDR imeeleza mipango yake ya kuongeza uwezo wa reli hiyo wa kubeba mizigo kutoka tani milioni mbili za sasa hadi tani milioni 6.2 ifikapo mwaka 2027 na hatimaye reli hiyo kuweza kushughulikia angalau asilimia 25 ya jumla ya biashara ya kuagiza na kuuza nje ya Ethiopia.

Ikiashiria umuhimu wa kimkakati unaongezeka wa reli, EDR imesema shughuli zake zimejikita katika huduma za ongezeko la thamani kama vile usafiri wa njia nyingi, usambazaji wa mizigo, uhifadhi wa mizigo, vibali vya forodha, na huduma za abiria, ili kusaidia kuunda upya usafirishaji kati ya Ethiopia na Djibouti.

Ikiwa imejengwa kwa pamoja na Kampuni ya Uhandisi wa Reli ya China na Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi ya China, reli hiyo ya kilometa 752, inayojulikana pia kama Reli ya Addis Ababa-Djibouti, ni njia ya kwanza ya reli ya kuvuka mpaka barani Afrika inayotumia umeme.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha