Rais Xi ahimiza wanakijiji mkoani Xizang, China kudumisha mshikamano wa makabila

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) kwenye barua ya majibu kwa wakazi wa kijiji cha Nyingchi, ambako alifanya ziara Julai 2021 amehimiza wakazi wa kijiji hicho kilichoko Mkoa unaojiendesha wa Xizang kudumisha mshikamano wa makabila na kujenga maisha bora ya furaha zaidi.

Rais Xi amesema, "nimeambiwa kwamba mabadiliko mapya yametokea katika kijijini miaka ya hivi karibuni na mapato ya wanakijiji yameongezeka, nimefurahi kwa hayo yote".

Rais Xi pia ameeleza matumaini yake kwamba wanakijiji, chini ya mwongozo wa sera za Chama za kuendeleza maeneo ya mpakani na kuboresha maisha ya watu, watalinda vizuri zaidi mandhari mazuri ya mazingira ya asili ya uwanda wa juu wa mkoa huo, kuendeleza chapa ya utalii ya kijiji hicho, na kutoa mchango kwa ajili ya ujenzi wa eneo la mpakani lenye ustawi na utulivu.

Kijiji hicho kinajulikana kwa maua ya peach yanayochanua vizuri. Katika miaka ya hivi karibuni, kijiji hicho kimepata mafanikio mapya katika kuendeleza shughuli za utalii kijijini, kuimarisha uchumi wa ushirika na kuhimiza mshikamano wa makabila.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha