

Lugha Nyingine
China na Vietnam zafanya mkutano wa mpaka juu ya ushirikiano wa kisheria
Picha hii iliyopigwa tarehe 28 Juni 2025 ikionyesha hafla ya ufunguzi wa mkutano wa mpaka uliofanywa na mamlaka za utawala wa Kisheria kutoka China na Vietnam, mjini Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Yin Gang)
NANNING - Mamlaka za utawala za kisheria kutoka China na Vietnam zimefanya mkutano wa mpaka kuanzia Jumamosi hadi jana Jumapili mjini Nanning, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, ili kuimarisha ushirikiano ambapo mkutano huo, wa kwanza wa aina yake, umekutanisha pamoja washiriki karibu 150 kutoka nchi zote mbili, wakiwemo maafisa kutoka idara za sheria, vyombo vya utawala wa kisheria vya nchi husika na wanataaluma wa sheria.
Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimefikia maafikiano mapana juu ya kuanzisha njia mbalimbali za kutatua migogoro ya kiraia na kibiashara kwenye mpaka, kupanua ushirikiano wa huduma za kisheria, na kwa pamoja kuwaandaa watu wenye ujuzi wa kisheria.
Waziri wa Sheria wa China He Rong amesema nchi hizo mbili zitafanya kazi pamoja kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa kivitendo katika masuala kama vile utungaji sheria, huduma za kisheria, msaada wa kisheria, mafunzo ya watu na matumizi ya teknolojia za kidijitali.
Waziri wa Sheria wa Vietnam Nguyen Hai Ninh amesema mkutano huo utasaidia kujenga mpaka wenye amani na wa kirafiki, kuzidisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili, na kwa pamoja kuhimiza ujenzi wa jumuiya muhimu ya kimkakati ya Vietnam na China yenye mustakabali wa pamoja.
Washiriki pia wameshiriki katika majadiliano ya kina kuhusu huduma za wanasheria, upatanishi, ushirikiano wa kimataifa, msaada wa kisheria kuhusu mambo ya kiraia na ya kibiashara, na kuwanandaa watu wenye ujuzi wa kisheria.
Pia makubaliano kadhaa ya ushirikiano yametiwa saini wakati wa mkutano huo.
Picha hii iliyopigwa tarehe 28 Juni 2025 ikionyesha hafla ya kutia saini makubaliano ya ushirikiano kwenye mkutano wa mpaka uliofanywa na mamlaka za utawala wa Kisheria kutoka China na Vietnam, mjini Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Yin Gang)
Picha hii iliyopigwa tarehe 28 Juni 2025 ikionyesha hafla ya kutia saini makubaliano ya ushirikiano kwenye mkutano wa mpaka uliofanywa na mamlaka za utawala wa Kisheria kutoka China na Vietnam, mjini Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Yin Gang)
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma