

Lugha Nyingine
Tanzania yazindua huduma za usafirishaji mizigo kwa treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza rasmi shughuli za usafirishaji mizigo kwa treni zake zinazotumia umeme za SGR, kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Utoaji huduma hiyo ya kusafirisha mizigo unafuatia kukamilika kwa mafanikio majaribio mapema mwaka huu, ambayo yalihusisha mabehewa 264 ya mizigo yaliyotengenezwa nchini China.
TRC imesema katika taarifa yake ya Ijumaa kwamba treni hiyo ya kwanza ya mizigo iliyojumuisha mabehewa 10 na kusafirisha zaidi ya tani 700 za bidhaa mbalimbali, iliondoka Dar es Salaam saa 10:35 alfajiri na ilikuwa ikitarajiwa kufika Dodoma saa nane mchana siku hiyohiyo ya Ijumaa.
Kati ya mabehewa 264 ya awali, 200 yametengwa kwa ajili ya usafirishaji wa makontena, 64 yaliyobaki ni kwa ajili ya kubeba mizigo midogo midogo.
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma