Shauku ya kujifunza lugha ya Kichina yaongezeka katika madarasa ya Ghana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2025

Wanafunzi wakihudhuria darasa la lugha ya Kichina katika Shule ya Kimataifa ya Penuel mjini Kasoa katika Mkoa wa Kati, Ghana, Juni 25, 2025. (Xinhua/Seth)

Wanafunzi wakihudhuria darasa la lugha ya Kichina katika Shule ya Kimataifa ya Penuel mjini Kasoa katika Mkoa wa Kati, Ghana, Juni 25, 2025. (Xinhua/Seth)

ACCRA - Huku uhusiano kati ya China na Ghana ukizidi kuwa wa kina, shauku ya kujifunza lugha ya Kichina inaenea kwa kasi katika shule mbalimbali za Ghana, ikionyesha ushirikiano mpana wa kiutamaduni na kielimu kati ya pande hizo mbili.

Katika mstari wa mbele wa mwelekeo huo ni Shule ya Kimataifa ya Penuel mjini Kasoa katika Mkoa wa Kati wa Ghana, ambapo wanafunzi wanapenda lugha ya Kichina, wakichochewa na fursa za mawasiliano ya kiutamaduni na matarajio ya kitaaluma katika siku za baadaye.

Asubuhi ya Jumatano katika Shule ya Kimataifa ya Penuel, iliyoko umbali wa kilomita takriban 35 magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo Accra, wanafunzi walikuwa wamezama katika masomo yao ya lugha ya Kichina. Katika darasa moja, Cai Leqin, mwalimu mchina aliyepangiwa kazi na Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Cape Coast (CIUCC), anaongoza darasani.

Kwa msisimko dhahiri, wanafunzi hurudia sentensi za Kichina kwa pamoja. Wengine wakijitambulisha kwa zamu katika lugha hiyo ya Kichina, huku wengine wakitafsiri msamiati wa lugha ya Kichina kwenda Kiingereza.

"Ninaona kujifunza lugha ya Kichina kuwa jambo la kusisimua na lenye manufaa kwa sababu inatusaidia kuelewa utamaduni wao," amesema Cheryl Abban, mmoja wa wanafunzi, ambaye anatamani kuwa mwanasheria na anatarajia kusoma nchini China na anaona kujifunza lugha hiyo kama njia bora ya kuwasiliana na kujijumuisha katika jamii ya Kichina.

Kwa kutambua ushawishi duniani unaokua wa China, bodi ya shule na jumuiya ya wazazi na walimu iliidhinisha pendekezo mwaka 2018 la kuanzisha madarasa ya lugha ya Kichina. Mkataba wa maelewano ulitiwa saini na CIUCC, ambayo sasa mara kwa mara hutuma walimu Wachina na wale wenyeji wa Ghana waliofunzwa kuunga mkono mpango huo, amesema mkurugenzi wa shule hiyo, Alex Lavoe.

Anastasia Appiah, mwanafunzi katika darasa hilo, anahamasishwa na Ufadhili wa Masomo wa Balozi wa China, ambao hutoa tuzo za fedha kwa ufaulu bora katika masomo ya lugha ya Kichina.

"Kujifunza lugha ya Kichina kunakupa fursa nyingi, ikiwemo kushiriki katika mashindano ya Daraja la Lugha ya Kichina. Ukishinda, unapata udhamini kamili wa kutembelea China. Hali hiyo inaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha yako," Anastasia amesema.

Mwalimu huyo mchina Cai anasema amefurahishwa na maendeleo ya wanafunzi wake. "Kichina ni lugha ngumu, lakini wanajitahidi kadri wawezavyo kujifunza shuleni na baada ya shule vilevile," anasema.

Kwa mujibu wa Lavoe, kuanzishwa kwa masomo ya lugha ya Kichina kumeongeza sana umaarufu wa shule hiyo. "Awali, udaili ulikuwa wanafunzi 420. Baada ya shule kuanzisha somo la lugha ya Kichina, umeongezeka hadi wanafunzi 720 ndani ya miezi minne. Kisha hadi 900, na sasa tumevuka 1,000," amesema.

Ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka, shule hiyo pia inajiandaa kuzindua madarasa ya lugha ya Kichina kwa watu wazima, hasa kwa wale wanaofanya biashara na China au wanaosafiri huko mara kwa mara.

Mwalimu mchina Cai Leqin (katikati) akionyesha kazi ya sanaa ya kukata karatasi ya Kichina kwa wanafunzi katika Shule ya Kimataifa ya Penuel mjini Kasoa katika Mkoa wa Kati, Ghana, Juni 25, 2025. (Xinhua/Seth)

Mwalimu mchina Cai Leqin (katikati) akionyesha kazi ya sanaa ya kukata karatasi ya Kichina kwa wanafunzi katika Shule ya Kimataifa ya Penuel mjini Kasoa katika Mkoa wa Kati, Ghana, Juni 25, 2025. (Xinhua/Seth)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha