

Lugha Nyingine
Programu ya mafunzo ya dawa za jadi za China yazinduliwa nchini Sierra Leone
Mwanafunzi (kushoto) akifanya mazoezi ya vitendo ya tiba ya acupuncture chini ya mwongozo wa mtaalamu kutoka timu ya madaktari wa China wakati wa kozi ya mafunzo juu ya mbinu za dawa za jadi za China (TCM) mjini Freetown, Sierra Leone, Juni 27, 2025. (Kundi la 26 la timu ya madaktari wa China nchini Sierra Leone/kupitia Xinhua)
REETOWN - Kundi la 26 la timu ya madaktari wa China nchini Sierra Leone limefanya mafunzo ya mbinu za dawa za jadi za China (TCM) mjini Freetown, mji mkuu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika, kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa, ambapo ikiwa na washiriki zaidi ya 80, programu hiyo ya siku mbili imetumika kama hatua ya kivitendo kuelekea kuimarisha ushirikiano wa huduma za afya kati ya China na Sierra Leone wakati huohuo kuhimiza ujumuishaji wa TCM kwenye mifumo ya afya ya nchi hiyo.
Liu Longfei, mkuu wa timu hiyo ya madaktari wa China, amesema mbinu yao inajumuisha TCM na desturi za kisasa za tiba za Magharibi kuunda suluhu za kina kwa wagonjwa.
Amesema, lengo kuu la programu hiyo ya mafunzo lilikuwa kutoa maelekezo mahsusi katika mbinu muhimu za TCM, ikiwemo nadharia ya meridian, acupuncture, tuina (masaji ya matibabu) na tiba ya kikombe.
"Hasa, tunazingatia katika matumizi ya kimatibabu mahsusi kwa ajili ya kushughulikia tatizo la kupasuka kwa diski kweye kiuno (lumbar disc herniation), ambayo ni ya kawaida hapa Sierra Leone," amesema Liu.
Kwa mujibu wa Liu, washiriki watakaofaulu tathmini ya mwisho watapokea cheti rasmi cha TCM na wanaweza kufuzu kwa fursa za matibabu katika Kituo cha TCM cha Hospitali ya Urafiki kati ya China-Sierra Leone.
Liu amesisitiza umuhimu wa kukuza wataalamu wa huduma ya afya waliobobea katika mbinu za TCM, kwa lengo la kujenga nguvukazi endelevu ya huduma ya afya yenye uwezo wa kuhudumia jamii zao kwa kujitegemea.
Wafanyakazi wenyeji wa matibabu wakijifunza kwa kutazama huku daktari mchina (wa kwanza, kushoto) akitibu mgonjwa wakati wa kozi ya mafunzo juu ya mbinu za dawa za jadi za China (TCM) mjini Freetown, Sierra Leone, Juni 27, 2025. (Kundi la 26 la timu ya madaktari wa China nchini Sierra Leone/kupitia Xinhua)
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma