Rais wa Botswana ahimiza kampuni zinazomilikiwa na serikali kutafuta fursa kwenye masoko ya kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2025

Rais Duma Boko wa Botswana (mbele) akizungumza kwenye mkutano na watendaji wa kampuni zinazomilikiwa na serikali (SOEs) na mashirika ya umma mjini Gaborone, Botswana, Juni 30, 2025. (Xinhua/Guo Chunju)

GABORONE - Rais Duma Boko wa Botswana jana Jumatatu kwenye mkutano na watendaji wa kampuni zinazomilikiwa na serikali (SOEs) na mashirika ya umma mjini Gaborone, mji mkuu wa Botswana, amehimiza kampuni na mashirika hayo ya umma kuongeza tija na faida na kutafuta fursa kwenye masoko ya kimataifa, akitoa wito wa mageuzi ili kuhakikisha kuwa vyombo hivyo vinafanya kazi kama mashirika ya kujitegemea na yenye faida.

"SOEs lazima zikumbatie teknolojia, ufanisi, na uvumbuzi ili kufikia ushindani wa kimataifa," amesema.

Rais Boko amesema serikali imeanza kuandaa Mpango wa Taifa wa Mageuzi (NTP), mpango wa kina, unaoongozwa na wataalam ulioundwa kuharakisha maendeleo ya Botswana.

"NTP ina msingi juu ya utekelezaji na inazingatia hatua maalum za wizara na mashirika mbalimbali, zikiwemo SOEs na mashirika ya umma," ameongeza.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais wa Botswana, Moeti Mohwasa amezungumzia umuhimu wa kipekee wa SOEs, akisisitiza haja ya yenyewe kutumia unyumbulikaji, uwajibikaji, na usimamizi bora ili kutoa thamani halisi kwa nchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, SOEs zinakuwepo katika sekta za usafiri, nishati, mawasiliano, na huduma za kifedha, zikiwemo benki za rejareja na ufadhili wa maendeleo, nchini Botswana.

Rais Duma Boko wa Botswana (kwenye mimbari) akizungumza kwenye mkutano na watendaji wa kampuni zinazomilikiwa na serikali (SOEs) na mashirika ya umma mjini Gaborone, Botswana, Juni 30, 2025. (Xinhua/Guo Chunju)

Rais Duma Boko wa Botswana akizungumza kwenye mkutano na watendaji wa kampuni zinazomilikiwa na serikali (SOEs) na mashirika ya umma mjini Gaborone, Botswana, Juni 30, 2025. (Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Rais Duma Boko wa Botswana akizungumza kwenye mkutano na watendaji wa kampuni zinazomilikiwa na serikali (SOEs) na mashirika ya umma mjini Gaborone, Botswana, Juni 30, 2025. (Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha