China yasema Hong Kong ina mustakabali mpana na wenye matumaini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 02, 2025

BEIJING - Kutokana na uungwaji mkono thabiti wa nchi mama, utekelezaji thabiti wa sera ya "nchi moja, mifumo miwili", dhamira ya serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (SAR), na juhudi za pamoja za sekta mbalimbali za jamii, Hong Kong ina mustakabali mpana na wenye matumaini, Mao Ning, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema jana Jumanne.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mao amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu kutangazwa na kutekelezwa kwa Sheria ya Kulinda Usalama wa Taifa katika Hong Kong, mfumokazi wa kisheria wa Hong Kong umeimarishwa, utulivu na umoja wa kijamii vimeboreshwa, na haki na uhuru wa wakazi wa Hong Kong kwa mujibu wa sheria umelindwa kikamilifu.

Mao amesema upakaji matope usio na msingi na wa nia mbaya unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wa nchi za Magharibi na mashirika yanayoipinga China dhidi ya "nchi moja, mifumo miwili," pamoja na mashambulizi yao dhidi ya utawala wa sheria wa Hong Kong, vinafichua kikamilifu nia yao mbaya ya kudhoofisha utulivu katika Hong Kong.

Amesema kuwa kutokana na kiwango cha juu cha usalama, Hong Kong inaweza kufikia maendeleo bora ya hali ya juu na Pato la Jumla la mkoa huo limekuwa likiongezeka kwa robo tisa mfululizo, akiongeza kuwa imeorodheshwa miongoni mwa vituo vitatu bora vya juu vya mambo ya fedha vya kimataifa duniani, na imepata tena nafasi tatu bora katika sehemu yenye nguvu kubwa za ushindani duniani.

"Ikiwa ni sehemu ya tatu inayopokea uwekezaji wa kigeni mwingi zaidi wa moja kwa moja duniani, Hong Kong inaongoza duniani katika kukusanya fedha kutoka kwenye IPOs tangu mwanzoni mwa mwaka huu, inashika nafasi ya kwanza duniani katika usafirishaji wa shehena za mizigo kwa anga na ya nne katika Fahirisi ya Maendeleo ya Kituo cha Kimataifa cha Uchukuzi wa Majini, na ni miongoni mwa 10 bora katika ushindani wa vipaji, huku mashirikisho mengi ya wafanyabiashara ya kigeni yakipendekeza kuongeza uwekezaji katika mji huo," Mao amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha