Uwanja wa ndege mkubwa zaidi wa Beijing wajiandaa kwa pilika nyingi za watalii wa majira ya joto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 02, 2025

Mtalii wa kigeni akipitia  utaratibu wa forodha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daxing  wa Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 27, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

Mtalii wa kigeni akipitia utaratibu wa forodha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daxing wa Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 27, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING - Uwanja wa ndege wa kimataifa wa wa Daxing wa Beijing ni uwanja mkubwa zaidi wa ndege katika mji mkuu huo wa China, umekadiria kusafirisha abiria zaidi ya milioni 9.52 katika kipindi cha pilika nyingi za utalii wa majira ya joto cha Julai-Agosti ambapo kuanzia Julai 1 hadi Agosti 31, uwanja huo unatarajia kushughulikia safiri 60,400 za ndege, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.18 kuliko mwaka uliopita.

Makadirio yanaonesha kuwa, idadi ya abiria inakadiriwa kufika milioni 9.52, kufikia ongezeko la asilimia 4.41 kuliko mwaka 2024. Na kipindi cha pilika nyingi zaidi za usafiri wa ndege kinatarajiwa kuwa ni Agosti 5, ambapo kutakuwa na usafiri wa ndege mara 1,031 na abiria 170,500 watakaopita kwenye uwanja huo wa ndege wa mji mkuu wa China.

Wasimamizi wa uwanja huo walisema, ongezeko hilo linatokana na mahitaji ya utalii wa mapumziko, kujumuika kwa familia na usafiri wa pamoja wa wafamilia.

Kwa mujibu wa rejea za oda za tiketi, kwa ndani ya China, njia maarufu zitaunganisha watu kwenye maeneo yenye hali iliyopoa ya majira ya joto kaskazini mashariki na kusini magharibi mwa China, pamoja na maeneo yenye vivutio vya utalii.

Aidha, oda hizo za tiketi zinaonesha kuwa, wasafiri wanaokwenda nje ya nchi wanapendelea maeneo ya safari fupi katika Asia Kusini-Mashariki na Asia Mashariki, wakati miji ya Ulaya kama London, Moscow na Amsterdam pia inaripoti kuongezeka kwa oda za tiketi na uhifadhi malazi.

Sera wezeshi za visa zimeharakisha utalii wa kuvuka mipaka ambapo katika kipindi cha majira ya joto, uwanja huo wa ndege wa Daxing unakadiria kuwa utashuhudia wastani wa kila siku wa karibu usafiri wa ndege wa kimataifa 100 na watu 17,000 kuvuka mpaka.

Imeelezwa kuwa, tangu Januari, uwanja huo wa ndege umesafirisha abiria zaidi ya milioni 2.7 wanaofanya utalii nje ya nchi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha