Mafanikio ya China katika uchapishaji wa 3D wa mwezi yafungua njia ya ujenzi wa "nyumba" mwezini kwa kutumia udongo wa mwezi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 02, 2025

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe ikimwonyesha mtafiti akionyesha mchakato wa uchapishaji wa 3D wa mwezi katika Maabara ya Uchunguzi wa Kina wa Anga ya Juu mjini Hefei, Mkoani Anhui, mashariki mwa China. (Xinhua)

Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe ikimwonyesha mtafiti akionyesha mchakato wa uchapishaji wa 3D wa mwezi katika Maabara ya Uchunguzi wa Kina wa Anga ya Juu mjini Hefei, Mkoani Anhui, mashariki mwa China. (Xinhua)

HEFEI - Mfumo wenye mafanikio wa uchapishaji wa 3D ulioundwa na wanasayansi wa China katika Maabara ya Uchunguzi wa Kina wa Anga ya Juu (Space) mjini Hefei, Mkoani Anhui umegundua njia ya kutumia udongo wa mwezini unaochukuliwa kutoka kwenye eneo husika la mwezini kwa ajili ya kujenga makazi, ikitengeneza njia kwa ajili ya ujenzi mkubwa, kwenye eneo husika la mwezini wa vituo vya utafiti wa mwezi.

Wanasayansi hao, wamefanikiwa kutoa kichapisho cha regolithi ya 3D ya mwezi ambacho kinaondoa hitaji la nyenzo za ujenzi zinazochukuliwa kutoka duniani, Yang Honglun, mhandisi mkuu katika maabara hiyo amesema.

Amesema kuwa mfumo huo unatumia kifaa cha kiakisi cha usahihi wa hali ya juu na upitishaji wenye kunyumbulika wa nishati ya fiber-optiki ili kufikia halijoto ya kutosha kuunganisha regolithi ya mwezi.

"Mafanikio haya ya uchapishaji yamethibitisha uwezekano wa kutumia udongo wa mwezini kama nyenzo pekee ya ujenzi, kuwezesha matumizi ya rasilimali za eneo husika la mwezi na kuondoa hitaji la kusafirisha nyenzo zozote nyingine kutoka duniani," amesema.

Pia miongoni mwa uvumbuzi muhimu wa mfumo huo wa uchapishaji ni utengenezaji nyumbulika, ambao huwezesha utengenezaji matofali na uchongaji mahsusi wa maumbo wa miundo tata, Yang ameeleza

“Jaribio la awali la mchakato wa kuunda regolithi ya mwezi ya mfano limekamilika kwenye ardhi.” ameongeza.

Amefafanua kuwa, katika hatua za awali za kazi ya timu ya watafiti, changamoto kubwa ilikuwa kutimiza mkusanyiko wa nishati ya jua na uundaji wa regolithi chini ya hali mbaya ya mazingira ya mwezini.

“Baada ya majaribio ya kina, timu hiyo ya fani mbalimbali -- zinazohusu nyanja za sayansi ya sayari, sayansi ya nyenzo, uhandisi wa mitambo, mienendo ya nishati, fizikia ya joto na optiki - imetatua masuala muhimu katika kukamata na kusambaza nishati, na uundaji maumbo” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha