Rais Xi ahimiza mashirikisho ya vijana na wanafunzi kuzidisha mageuzi, uvumbuzi kwa mafanikio mapya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito kwa mashirikisho ya vijana na wanafunzi wa China kufuata mwelekeo sahihi wa kisiasa, kuendeleza kwa kina mageuzi na uvumbuzi, na kufunga safari mpya ya kujipatia mafanikio mapya chini ya uongozi wa Chama.

Rais Xi, amesema hayo katika barua ya pongezi kwa mkutano wa Shirikisho Kuu la Vijana wa China na Shirikisho Kuu la Wanafunzi wa China, uliofunguliwa jana Jumatano asubuhi Beijing.

Rais Xi akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, ametoa pongezi na salamu kwa vijana wa makabila yote na wa sekta mbalimbali, na vijana wanafunzi wa China walioko ng'ambo.

"Katika miaka mitano iliyopita, mashirikisho ya vijana na wanafunzi ya ngazi zote yametekeleza ipasavyo majukumu yao, yakionyesha sura yao ya vijana wanaoinua vifua juu kwa kujikakamua, na kufanya juhudi kubwa za nguvu ya vijana wa China wa kizazi kipya,” Rais Xi amesema katika barua hiyo.

Amesema kuwa vijana wana jukumu kubwa la kufanya wakati China inapojitahidi kujenga nchi yenye nguvu na kufikia ustawishaji wa taifa kwa pande zote kwa kupitia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, vijana wanapaswa kushikilia kithabiti matumaini na imani yao, kujenga hisia ya kuwajibika kwa nchi, na kubeba jukumu lao la kihistoria.

Rais Xi amezitaka oganaizesheni za Chama za ngazi zote kuimarisha uongozi wao wa kazi ya vijana, kuunga mkono kazi ya mashirikisho ya vijana na wanafunzi, na kuweka mazingira mazuri kwa ukuaji mzuri wa vijana na wanafunzi ili waweze kujiendeleza vizuri, na kujipata mafanikio mapya.

Cai Qi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, alihudhuria ufunguzi wa mkutano uliohudhuriwa na vijana na wanafunzi wapatao 3,000.

Mkutano wa Shirikisho Kuu la Vijana wa China na Shirikisho Kuu la Wanafunzi wa China   ukifunguliwa  Beijing, mji mkuu wa China, Julai 2, 2025. (Xinhua/Li Tao)

Mkutano wa Shirikisho Kuu la Vijana wa China na Shirikisho Kuu la Wanafunzi wa China ukifunguliwa Beijing, mji mkuu wa China, Julai 2, 2025. (Xinhua/Li Tao)

Mkutano wa Shirikisho Kuu la Vijana wa China na Shirikisho Kuu la Wanafunzi wa China  ukifunguliwa Beijing, Julai 2, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Mkutano wa Shirikisho Kuu la Vijana wa China na Shirikisho Kuu la Wanafunzi wa China ukifunguliwa Beijing, Julai 2, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC alihutubia mkutano huo kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC.

Mkutano wa Shirikisho Kuu la Vijana wa China na Shirikisho Kuu la Wanafunzi wa China   ukifunguliwa Beijing, Julai 2, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Mkutano wa Shirikisho Kuu la Vijana wa China na Shirikisho Kuu la Wanafunzi wa China ukifunguliwa Beijing, Julai 2, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Akisema kwamba barua hiyo ya pongezi ya Rais Xi imetoa mwongozo muhimu wa kusukuma mbele maendeleo ya harakati za vijana wa China, Li amesisitiza umuhimu wa kuelewa kwa kina na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Xi ili mafanikio makubwa zaidi yapatikane katika kazi ya Chama inayohusu vijana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha