China na EU zaahidi kushikilia mfumo wa pande nyingi na kuimarisha ushirikiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2025

Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mjini Brussels, Ubelgiji, Julai 2, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

BRUSSELS - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa wamekutana mjini Brussels, makao makuu ya Umoja wa Ulaya jana Jumatano, wakiahidi kushikilia mfumo wa pande nyingi na kuimarisha ushirikiano.

Akisema kuwa zote Umoja wa Ulaya (EU) na China ni waungaji mkono wa mfumo wa pande nyingi, Costa amesema EU inapenda kushirikiana na China ili kushikilia kuheshimiana, kuvuka tofauti, kuhimiza maelewano, na kwa pamoja kushughulikia changamoto za dunia.

"EU inapenda kushirikiana na China kuhakikisha mafanikio kamili ya mkutano ujao wa viongozi wa EU na China," amesema, akiongeza kuwa EU itaendelea kufuata bila kuyumba sera ya kuwepo kwa China moja.

Kwa upande wake, Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kuwa China inaichukulia Ulaya kama ncha muhimu katika dunia yenye ncha nyingi, na China siku zote imekuwa ikiunga mkono muungano wa Ulaya na inafurahi kuona EU ikiimarisha kujitegemea kwake kimkakati na kubeba jukumu kubwa zaidi katika jukwaa la kimataifa.

Wang amesema China inapenda kuimarisha mawasiliano na uratibu na EU na kujiandaa kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya.

"Kadiri hali mbaya na ngumu ya kimataifa inavyozidi kuwa, ndivyo China na EU zinavyohitaji kuimarisha mshikamano na uratibu, na kuchukua hatua kithabiti kama nguvu za kutuliza hali katika dunia yenye misukosuko," Wang amesema, akiongeza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kuheshimu kwa dhati maslahi ya msingi ya kila upande, kuongeza maelewano na hali ya kuaminiana, na kutoa mchango katika mafanikio ya kila upande.

Pande hizo mbili pia zilibadilishana maoni kuhusu mgogoro wa Ukraine.

Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mjini Brussels, Ubelgiji, Julai 2, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mjini Brussels, Ubelgiji, Julai 2, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha