Sudan Kusini yaanzisha mradi wa dola za kimarekani milioni 58 kuendeleza watoto shuleni

(CRI Online) Julai 03, 2025

Sudan Kusini imeanzisha mradi wa miaka minne wa kuhimiza upatikanaji wa elimu bora na jumuishi na kuboresha matokeo ya mafunzo kwa ajili ya watoto haswa wa kike na wanaoishi katika mazingira duni.

Mradi huo uliofadhiliwa na Mfuko wa Ushirikiano wa Kimataifa kwa Elimu (GPE) utatekelezwa kwa pamoja na serikali ya Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada, na unatarajiwa kunufaisha watoto zaidi ya laki tatu moja kwa moja na wengine laki sita kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika kaunti 20 nchini humo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Sudan Kusini Kuyok Abol Kuyok, amesema ufadhili huo utatoa nafasi za upatikanaji wa elimu inayohitajika kwa watoto walioathiriwa na migogoro inayoendelea nchini humo, huku akitoa wito kwa viongozi wa jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada husika ili kudumisha mwelekeo huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha