Wavumbuzi wa Tanzania watengeneza jukwaa la AI ili kukabiliana na masuala ya afya ya akili

(CRI Online) Julai 03, 2025

Wakati masuala ya afya ya akili yakiongezeka nchini Tanzania, timu ya wavumbuzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) imeunda jukwaa la Akili Mnemba (AI) linalolenga kutambua mapema dalili za matatizo ya afya ya akili na kuwaelekeza watumiaji kupata usaidizi kwa wakati.

Jukwaa hilo linalojulikana kwa jina la Akili Check, kwa sasa lipo katika hatua ya majaribio katika hospitali nne za rufaa: Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Benjamin Mkapa, Hospitali ya Milembe na Hospitali ya Amana.

Akizungumzwa kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea ambako uvumbuzi huo unaoneshwa kwa umma, mtafiti mkuu Bw Kukwa Malyango alisema Jumanne kuwa wagonjwa wengi wanaishia kwenye vituo vya afya ya akili kutokana na ukosefu wa zana za kutathmini mapema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha