Uganda yaagiza mbuzi chotara kutoka China kukuza sekta ya mifugo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2025

Mtaalamu mchina akimchunga mbuzi Jianzhou mwenye masikio makubwa kwenye zizi katika Kituo cha Taifa cha Rasilimali za Jenetiki za Wanyama na Hifadhi ya Data (NAGRC&DB) mjini Entebbe, Uganda, Julai 1, 2025. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

ENTEBBE, Uganda - Mbuzi tisa chotara kutoka China, wanaojulikana pia kwa jina la mbuzi Jianzhou wenye masikio makubwa, wamewasili Uganda wakati ambapo nchi hiyo ya Afrika Mashariki ikitafuta kukuza uzalishaji nyama ya mbuzi na sekta ya mifugo ambapo mbuzi hao -- madume watatu na majike sita -- walitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe juzi Jumatatu usiku baada ya safari ya saa zaidi ya 10 kutoka Chengdu, Mkoa wa Sichuan, Magharibi mwa China.

Kama jamii ya wanyama chotara kati ya mbuzi wa Kinubi wa Uingereza na mbuzi wa kienyeji wa Jianyang, hii ni mara ya kwanza kwa mbuzi hao Jianzhou wenye masikio makubwa kusafirishwa nje ya China.

Wanyama hao wameagizwa kuingia nchini humo chini ya Mradi wa Ushirikiano wa Kusini na Kusini kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, China na Uganda, mpango wa pande tatu unaolenga kuhamisha teknolojia ya kilimo na mbinu bora kutoka China hadi Uganda.

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo, wanyama na Uvuvi ya Uganda (MAAIF), mradi huo unazingatia uzalishaji mazao, ufugaji samaki, na uboreshaji wa mifugo ambapo chini ya kipengele chake cha ufugaji, mbuzi huyo Jianzhou mwenye masikio makubwa ametambuliwa kama aina muhimu ya kusaidia kuifanyia mageuzi sekta ya ufugaji wa mbuzi ya Uganda.

Rose Ademun, kamishna wa afya ya wanyama katika MAAIF, amesema mbuzi huyo Jianzhou mwenye masikio makubwa ni "mbegu bora ya nyama inayojulikana kwa ukuaji wake wa haraka, mavuno mengi ya mzoga, na kubadilika kuendana na hali mbalimbali za hali ya hewa ya kilimo.”

Ademun ameyasema hayo alipohojiwa na Shirika la Habari la China, Xinhua siku ya Jumanne katika Kituo cha Taifa cha Rasilimali za Jenetiki za Mifugo na Hifadhi ya Data (NAGRC&DB), ambapo mbuzi hao walioagizwa kutoka China wanafugwa na watapitia awamu ya utafiti na uzalishaji kuongeza idadi yake.

"Mbali na kuongeza uzalishaji nyama, mbuzi hao walioagizwa kutoka China pia watatumika kuchanganya mbegu za uzazi na mbuzi wa kienyeji nchini humo ili kuboresha tija, hatimaye kuinua kipato cha wakulima," ameongeza Ademun, huku akiishukuru China kwa kuchangia mifugo hiyo.

Tangu mwaka 2012, chini ya mfumo wa ushirikiano wa pande tatu, China imekuwa ikituma wataalam wa kilimo kufanya kazi moja kwa moja na wakulima wa Uganda, wakitoa ujuzi na teknolojia. Katika sekta ya kulima mazao, wameanzisha aina zinazotoa mazao mengi kama vile mtama wa mkia wa mbweha na mpunga chotara, pamoja na utaalamu wa ufugaji wa samaki na ufugaji mifugo.

Maafisa na wataalamu wa kilimo wakiwakagua mbuzi Jianzhou wenye masikio makubwa walioagizwa hivi karibuni katika Kituo cha Taifa cha Rasilimali za Jenetiki za Wanyama na Hifadhi ya Data (NAGRC&DB) mjini Entebbe, Uganda, Julai 1, 2025. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Picha iliyopigwa Julai 1, 2025 ikiwaonyesha mbuzi Jianzhou wenye masikio makubwa walioagizwa hivi karibuni katika Kituo cha Taifa cha Rasilimali za Jenetiki za Wanyama na Hifadhi ya Data (NAGRC&DB) mjini Entebbe, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha