

Lugha Nyingine
Mafunzo yaongeza ujuzi wa Tiba ya Jadi ya China miongoni mwa wafanyakazi wa afya wa Niger
Madaktari wa timu ya 24 ya Wataalamu wa matibabu ya China nchini Niger wakitoa mafunzo kuhusu matibabu ya tiba za jadi za China katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Niamey, Niger, Juni 27, 2025. (Timu ya 24 ya wataalamu wa matibabu ya China nchini Niger/kupitia Xinhua)
NIAMEY - "Sindano ndogo ya fedha, inapotumiwa kwenye sehemu sahihi ya mwilini yenye maumivu, inaweza kuleta nafuu kubwa kwa wagonjwa, tumejionea hili kwa macho yetu," amesema Mamane Daou, mkurugenzi mkuu wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Niamey mjini Niamey, mji mkuu wa Niger.
Akizungumza kwenye mafunzo ya hivi karibuni iliyoandaliwa na hospitali yake, ameielezea mafunzo hayo kuwa fursa muhimu kwa wafanyakazi wa matibabu na umma kwa ujumla kupata ufahamu wa karibu juu ya mbinu hiyo ya tiba ya kale.
Wataalamu takriban 50 wa huduma ya afya kutoka Niger, wakiwemo wafanyakazi muhimu wa matibabu kutoka hospitali hiyo, wafanyakazi wa masomo kwa vitendo kutoka Kitivo cha Sayansi ya Afya cha Chuo Kikuu cha Abdou Moumouni na wapenda Tiba ya Jadi ya China (TCM), walishiriki katika mafunzo hayo juu ya mbinu za TCM iliyoandaliwa na timu ya 24 ya wataalamu wa matibabu ya China.
Mafunzo hayo yalianza kwa mhadhara wenye kichwa "Hekima ya Tiba ya Jadi ya China: Historia, Nadharia na Mitazamo ya Dunia" iliyowasilishwa na daktari wa China Wang Qingwu, ambaye alielezea maendeleo ya TCM na mfumokazi wake wa kinadharia, akifafanua juu ya maeneo ya mwilini yanayotumiwa mara kwa mara kwa tiba ya acupuncture na mbinu za tiba hiyo.
Washiriki wawili ambao walikuwa na tatizo la maumivu ya kichwa ya mara kwa mara na kufa ganzi mikononi walijitolea kwa ajili ya matibabu na walipata nafuu ya haraka, jambo ambalo liliwavutia washiriki wenzao.
"Tiba ya Jadi ya China ni rahisi, salama na bei nafuu, na tayari imewanufaisha wagonjwa wengi wa Niger," amesema Daou.
Niger inaweka umuhimu mkubwa sana katika kuendeleza dawa zake za kijadi, amesema, akielezea matumaini yake ya kuendelezwa ushirikiano na China ili kuimarisha uwepo na mustakabali wa TCM nchini humo.
Zheng Zhida, kiongozi wa timu hiyo ya matibabu ya China, amesema Kituo cha Uchunguzi na Tiba za TCM, kilichoanzishwa katika hospitali hiyo mwaka 2023, tayari kimetoa matibabu kwa maelfu ya wagonjwa, haswa katika kupona kiharusi na urejeshaji afya ya mwili baada ya watu kupata kiwewe.
"Mafunzo haya si tu kuhusu kuenzi ujuzi wa matibabu lakini pia ni kuhusu mawasiliano ya kiutamaduni. Tutaendelea kuhimiza tiba ya TCM kuendana na hali ya nchini humo ili kuwahudumia vema wakazi wa Niger." Zheng amesema.
Madaktari wa timu ya 24 ya wataalamu wa matibabu ya China nchini Niger wakitoa mafunzo kuhusu matibabu ya tiba za jadi za China katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Niamey, Niger, Juni 27, 2025. (Kundi la 34 la timu ya wataalamu wa matibabu ya China nchini Niger/kupitia Xinhua)
Madaktari wa timu ya 24 ya wataalamu wa matibabu ya China nchini Niger wakitoa mafunzo ya mazoezi ya Baduanjin katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Niamey, Niger, Juni 27, 2025. (Timu ya 24 ya wataalamu wa matibabu ya China nchini Niger/kupitia Xinhua)
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma