

Lugha Nyingine
Wataalamu wa Nchi za Kusini wakutana Yunnan, China kujadili uhifadhi na maendeleo ya urithi wa dunia
Wageni zaidi ya 120 kutoka nchi 24 za kundi la Nchi za Kusini Jumapili walikutana mjini Chengjiang katika Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, kujadili uhifadhi na maendeleo ya urithi wa dunia.
Wataalamu hao wamejumuika katika mkutano uliofanyika chini ya Kongamano la Vyombo vya Habari na Taasisi za Washauri Bingwa la Nchi za Kusini Mwaka 2025, lililoandaliwa kwa pamoja na Shirika la Habari la China, Xinhua, Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Serikali ya Mkoa wa Yunnan.
Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya CPC ya Mkoa wa Yunnan ambaye pia ni mkuu wa idara ya uenezi ya kamati hiyo, Zeng Yan amesema, Yunan ni nyumbani kwa maeneo sita ya urithi wa dunia, ambayo ni idadi ya pili kwa wingi nchini China.
Aidha, amesema ili kuhifadhi urithi huo inahitaji jitihada za pamoja huku juhudi zaidi zikiwekwa katika kuimarisha utafiti, mageuzi, mabadilishano na ushirikiano.
Naibu Mkuu wa Shirika la Habari la China, Xinhua Xi Yanchun amesema shirika hilo litaendelea kuimarisha ushirikiano na serikali, vyombo vya habari, na taasisi za washauri bingwa katika nchi za Kusini, na kuhimiza maelewano na mwamko wa umma juu ya uhifadhi na urithi wa dunia.
Naye Kiongozi wa Taasisi ya Imagindia, Robinder Nath Sachdev amesema, ingawa maeneo mengi ya urithi wa dunia ya nchi za Kusini yanatambuliwa duniani, lakini mitazamo ya nchi hizo bado haisikiki vizuri duniani.
Ametoa wito kwa kundi la Nchi za Kusini kuwa na sauti kubwa zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma