Kampuni kubwa ya betri ya CATL ya China yazindua betri mpya za EV kwa ajili ya Ulaya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 08, 2025

Picha hii ya kumbukumbu ikionyesha kampuni ya Contemporary Amperex ya Thuringia GmbH mjini Thuringia, Ujerumani. (CATL Ujerumani/kupitia Xinhua)

Picha hii ya kumbukumbu ikionyesha kampuni ya Contemporary Amperex ya Thuringia GmbH mjini Thuringia, Ujerumani. (CATL Ujerumani/kupitia Xinhua)

MUNICH, Ujerumani - Kampuni ya CATL ya China, kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza betri duniani, jana Jumapili imezindua betri za gari linalotumia umeme (EV) za kizazi kipya mjini Munich, Ujerumani, kwa ajili ya soko la Ulaya, ikionyesha ushawishi wake na dhamira yake inayoongezeka katika kanda hiyo.

Uzinduzi huo umekuja siku mbili kabla ya kufunguliwa kwa maonyesho ya Vyombo vya Usafiri ya IAA 2025 mjini Munich, mkusanyiko unaoongoza wa sekta ya magari barani Ulaya.

Betri hiyo mpya, iliyopewa jina la "Shenxing Pro," inategemea kemia ya lithiamu iron phosphate (LFP) na itatolewa katika matoleo mawili mahsusi kwa soko la Ulaya.

Toleo hilo la kudumu kwa muda mrefu limeundwa kudumu kwa hadi miaka 12 au kilomita milioni 1 za matumizi na unatoa kiwango cha juu cha kuendesha gari cha umbali wa kilomita 758, juu zaidi ya kiwango cha kilomita 300 hadi 500 ambacho kawaida hutolewa na betri za LFP. Toleo lingine ni la muundo wa kuchajiwa kwa haraka, ambalo linaweza kuongeza umbali wa kilomita 478 kwa kuchajiwa dakika 10 tu.

Picha hii ikionyesha Betri Shenxing ya Kuchajiwa haraka Sana inayoonyeshwa kwenye banda la Kampuni ya Teknolojia ya Contemporary Amperex (CATL) wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Magari 2023, yanayojulikana rasmi kwa jina la IAA MOBILITY 2023, mjini Munich, Ujerumani, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Zhang Fan)

Picha hii ikionyesha Betri Shenxing ya Kuchajiwa haraka Sana inayoonyeshwa kwenye banda la Kampuni ya Teknolojia ya Contemporary Amperex (CATL) wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Magari 2023, yanayojulikana rasmi kwa jina la IAA MOBILITY 2023, mjini Munich, Ujerumani, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Zhang Fan)

Lingbo Zhu, afisa mkuu wa teknolojia wa kitengo cha biashara ya kimataifa cha CATL, amesema bidhaa hiyo imeundwa kwa kuendana na tabia za madereva wa Ulaya, ikiwemo mwendo kasi katika barabara kuu, kudumu kwa muda mrefu kwa magari yaliyokodishwa na yaliyotumika, na ufanisi wa uhakika katika hali ya hewa ya baridi zaidi.

CATL iliingia katika soko la Ulaya mwaka 2012 kupitia ubia wa kimkakati na kampuni ya kuunda magari ya Ujerumani BMW. Sasa inaendesha viwanda vya kuzalisha EV nchini Ujerumani na Hungary, huku kiwanda cha tatu kikiwa kinajengwa nchini Hispania kupitia ubia na Stellantis.

"Safari yetu ya kimataifa inaanzia hapa Ulaya," amesema Tan Libin, afisa mkuu wa wateja wa CATL, akisema kuwa kampuni hiyo sasa inafanya ushirikiano na karibu asilimia 90 ya waundaji magari wa Ulaya.

Kwa mujibu wa Tan, CATL imetoa betri kwa zaidi ya magari milioni 20 ya umeme duniani kote. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha