China na AU zaahidi mshikamano ili kusukuma mbele amani na haki duniani

(CRI Online) Septemba 08, 2025

China na Umoja wa Afrika (AU) zimeahidi kuimarisha mshikamano katika kujenga mfumo wa utawala duniani ulio wa haki zaidi na dunia yenye amani.

Ahadi hiyo ilitolewa Ijumaa kwenye semina ya ngazi ya juu mjini Addis Ababa, Ethiopia, kwa ajili ya kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Wajapan na Vita vya Kupinga Ufashisti Duniani.

Akihutubia semina hiyo, mkuu wa ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika, Jiang Feng, amesisitiza umuhimu wa kukumbuka historia na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na changamoto za usalama zinazoikabili dunia.

Akizungumza kwa niaba ya kamishna wa AU wa Afya, Masuala ya Kibinadamu, na Maendeleo ya Jamii, mshauri mkuu wa kamishna huyo, Pamoussa Zackaria Konsimbo, amehimiza kuoanisha utawala wa dunia na kanuni za usawa, uhuru na ushirikiano wa kweli wa pande nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha