Mashindano ya Dunia ya Ujuzi kwa Shule za Ufundi Stadi Kanda ya Afrika yamalizika kwa mafanikio

(CRI Online) Septemba 08, 2025

Hafla ya kufunga na kutunuku medali katika Mashindano ya Dunia ya Ujuzi kwa Shule za Ufundi Stadi mwaka 2025 (Kanda ya Afrika) imefanyika kwa mafanikio katika Chuo cha Ufundi Stadi cha China-Zambia kilichopo mjini Luanshya, nchini Zambia.

Mashindano hayo yaliyofanyika Septemba 5 yamevutia timu 28 za shule za ufundi stadi kutoka Afrika Kusini, Nigeria, Tanzania, na Zambia, huku jumla ya wanafunzi 56 wakishiriki.

Baada ya ushindani mkali, timu ya Chuo cha Ufundi Stadi cha China-Zambia imeshinda medali za dhahabu katika Ufungaji na Uendeshaji wa Vifaa vya Mitambo ya Umeme, na Usanifu na Utengenezaji wa Mashine.

Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Zambia Felix Mutati amesema kuwa maendeleo ya ujuzi ni chachu katika kufikia uhuru wa kiuchumi na kuhimiza maendeleo endelevu.

Ametoa wito kwa vijana wa Afrika kuthamini fursa, kujifunza ujuzi, na kujenga kwa pamoja siku zijazo.

Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Ufundi na Watu Wazima katika Wizara ya Elimu ya China Li Zhi amesema katika hotuba yake kwa njia ya video kwamba Mashindano hayo yamefanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza na ameelezea matumaini yake kuwa mashindano hayo yatakuwa daraja la ujuzi la kuvuka mipaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha