

Lugha Nyingine
China na Tanzania kuimarisha uhusiano kupitia mashindano ya kombe la urafiki la mchezo wa tenisi ya mezani
China na Tanzania zimefanya mashindano ya kombe la urafiki ya tenisi ya mezani mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, yakikutanisha wachezaji, wanafunzi, wataalamu na Wachina wanaoishi nje ya nchi katika kusherehekea mabadilishano ya kimichezo na kiutamaduni.
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian alifungua mashindano hayo kwa mechi dhidi ya Rashid Sharif ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Tenisi ya Mezani Tanzania (TTTA), akitumia msemo maarufu wa Kichina usemao "Urafiki kwanza, halafu ndiyo mashindano" kuonesha msisitizo wa mashindano hayo
Mashindano hayo yaliyofadhiliwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania na Kituo cha Utamaduni cha China, na kuandaliwa na TTTA na Jumuiya ya Wafanyakazi wa Miradi inayofadhiliwa na China, yaliibua shauku kubwa ya ushiriki wa shule, vilabu vya michezo na taasisi.
Balozi Chen ameongeza kuwa sasa yakiwa katika msimu wa nne, mashindano hayo ya kombe la urafiki ya kila mwaka yamekua kwa kiwango na ushawishi wake, yakitoa ushindani na muunganisho.
Aidha amesema mashindano hayo yamekuwa jukwaa muhimu kwa watu wa China na Tanzania kuimarisha uhusiano wao kupitia michezo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma