

Lugha Nyingine
Rais Xi atoa mapendekezo matatu kwenye Mkutano wa viongozi wa BRICS wa mtandaoni ili kuimarisha mshikamano, kusukuma mbele ushirikiano
Rais wa China Xi Jinping akihudhuria Mkutano wa Mtandaoni wa Viongozi wa BRICS na kutoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kusonga Mbele katika Mshikamano na Ushirikiano" Septemba 8, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amehudhuria kwenye Mkutano wa mtandaoni wa Viongozi wa BRICS na kutoa hotuba muhimu, akitoa wito kwa nchi za BRICS kusonga mbele katika mshikamano na ushirikiano.
Mkutano huo wa mtandaoni wa viongozi uliofanyika jana Jumatatu uliongozwa na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na kuhudhuriwa pia na Rais wa Russia Vladimir Putin, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, Rais wa Indonesia Prabowo Subianto, Mrithi wa Kifalme wa Abu Dhabi Khaled bin Mohamed wa Umoja wa Falme za Kiarabu, na wajumbe wa India na Ethiopia.
Katika hotuba yake yenye kichwa cha "Kusonga Mbele katika Mshikamano na Ushirikiano," Rais Xi amesema kuwa hali ya mabadiliko ambayo hayajatokea katika miaka 100 iliyopita yanazidi kushamiria duniani kote, na umwamba, maamuzi ya upande mmoja, na kujilinda kibiashara vinazidi kutimua vumbi zaidi.
"Nchi za BRICS, zikiwa kwenye safu ya kwanza ya Nchi za Kusini, zinapaswa kushikilia kufuata moyo wa BRICS wa uwazi, ujumuishaji na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote, kwa pamoja kutetea mfumo wa pande nyingi na mfumo wa biashara wa pande nyingi, kusukuma mbele ushirikiano mkubwa zaidi wa BRICS, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja," Rais Xi amesema.
Ametoa mapendekezo matatu ili kufikia hilo.
Kwanza ametoa wito kwa nchi za BRICS kushikilia mfumo wa pande nyingi ili kutetea haki na usawa wa kimataifa. "Mfumo wa pande nyingi ni matarajio ya pamoja ya watu na mwelekeo mkuu wa zama tulizo nazo," ambao unatoa msingi muhimu kwa amani ya dunia na maendeleo ya dunia.
Rais wa China Xi Jinping akihudhuria Mkutano wa Mtandaoni wa Viongozi wa BRICS na kutoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kusonga Mbele katika Mshikamano na Ushirikiano" Septemba 8, 2025. (Xinhua/Liu Bin)
Pendekezo lake la pili ni kushikilia ufunguaji mlango na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote ili kulinda utaratibu wa kimataifa wa uchumi na biashara.
Huku akisema kuwa utandawazi wa uchumi duniani ni mwelekeo usiozuilika wa historia, nchi zote haziwezi kustawi bila mazingira ya kimataifa ya ufunguaji mlango na ushirikiano, na hakuna nchi inayoweza kurudi katika hali ya kujitenga peke yake.
Tatu, Rais Xi amesema, nchi za BRICS zinapaswa kushikilia mshikamano na ushirikiano ili kuhimiza matokeo ya maendeleo ya pamoja kutokana na uratibu na ushirikiano.
Rais Xi amesema, "idadi ya watu wa Nchi za BRICS inachukua karibu nusu ya idadi ya watu duniani, ukubwa wa uchumi wa nchi za BRICS ni karibu asilimia 30 wa uchumi wa dunia, na thamani ya jumla ya biashara ni moja ya tano ya biashara ya dunia," akiongeza kuwa, kama zikishikamana karibu zaidi, zitakuwa na nguvu zaidi za kukabiliana na hatari na changamoto, na kuonesha uthabiti, rasilimali na ufanisi zaidi.
Viongozi wengine waliohudhuria kwenye mkutano huo wamesema kuwa vitendo vya upande mmoja na umwamba vinaharibu utaratibu wa kimataifa, sheria na kanuni za kimataifa zinakabiliwa na tishio, na biashara inatumika kama chombo cha kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, hayo yote yanaathiri vibaya amani ya dunia na maendeleo ya dunia.
Viongozi hao wamesema kuwa Pendekezo la Usimamizi wa Dunia lililotolewa na Rais Xi ni muhimu na linaonyesha mwelekeo na njia wa kuboresha usimamizi wa Dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma