

Lugha Nyingine
Mashindano ya Ubunifu wa Video Fupi kuhusu Sikukuu ya Mbalamwezi ya China 2025 yaanzishwa
Mnamo tarehe 8, Septemba, mashindano ya ubunifu wa video fupi ya Guizhou Xijiu 2025, ambayo yaliandaliwa na kampuni ya pombe ya Guizhou Xijiu kwa kauli mbiu ya "Kunywa Pombe ya Xijiu wakati wa usiku wa Mbalamwezi" na "Picha na video za Mbalamwezi, kujumuika hapa China", yameanzishwa rasmi katika ukumbi wa studio No.1 wa People's Daily Online mjini Beijing, China.
Hali ya shughuli. (Picha/Peng Yunxi)
Mashindano hayo yanakaribisha kazi bora za video fupi kutoka watu wowote, yakilenga kuonesha furaha na upendo wa familia mbalimbali katika siku ya tarehe 5 ya mwezi wa tano kwa kalenda ya kilimo ya China, yaani Sikukuu ya Mbalamwezi ya China, ambayo ni moja kati ya sikukuu muhimu zaidi za jadi za China. Mashindano yameweka tuzo za aina nyingi na zaidi ya nafasi 40 za washindi wa tuzo. Watu wanaotaka kushiriki wanaweza kusoma maelezo husika ya mashindano kwenye tovuti yake, na kubuni video kwa kufuata matakwa.
Inafahamika kuwa muda wa kukusanya kazi umeanzia Agosti 8 hadi Oktoba 8, 2025, na hafla ya kutoa tuzo (“Usiku wa Wabunifu”) itafanyika Oktoba 23.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma