

Lugha Nyingine
Watu 10 wafariki, zaidi ya 40 wajeruhiwa baada ya basi la ghorofa mbili kugongwa na treni katikati mwa Mexico
Wafanyakazi wa uokoaji wakifanya kazi kwenye eneo la ajali katika mji wa Atlacomulco wa Jimbo la Mexico nchini Mexico, Septemba 8, 2025. (Picha na Francisco Canedo/Xinhua)
MEXICO CITY – Watu takriban 10 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa wakati basi la abiria lenye ghorofa mbili lilipogongwa na treni ya mizigo katikati mwa Mexico jana Jumatatu, ofisa mhusika amesema, ambapo mgongano huo umetokea kwenye barabara kuu ya serikali kuu ya Atlacomulco-Maravatio la Jimbo la Mexico, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Waliojeruhiwa wamekimbizwa hospitalini wakati huohuo mashirika ya dharura yalikuwa yakifanya kazi katika eneo la tukio, shirika la ulinzi wa raia la serikali limesema katika taarifa yake iliyotolewa majira ya saa 2:30 asubuhi kwa saa za Mexico, bila kutaja wakati halisi wa ajali.
Canadian Pacific Kansas City of Mexico, shirika mwendeshaji wa reli hiyo, limetoa rambirambi kwa familia za wafiwa baada ya kuthibitisha ajali hiyo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Wafanyakazi wake walikuwa wakishirikiana na mamlaka kwenye eneo la tukio na kutoa wito kwa umma kufuata alama za trafiki na kufuata alama za kusimama kwenye vivuko vya reli ili kuzuia ajali lisitokee, habari za vyombo vya habari zimesema.
Video ya mtandaoni inaonyesha kuwa kwenye barabara yenye pilika nyingi ambapo magari mengi yalikuwa yakingoja, basi hilo lenye ghorofa mbili polepole lilivuka reli na kisha kugongwa na treni hiyo na kusukumwa mbele kando ya reli.
Vyombo vya habari nchini humo vimesema, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la Mexico imeanzisha uchunguzi ili kuthibitisha hali ya mazingira ya ajali hiyo na kumpata dereva ambaye hakuwepo eneo la tukio.
Mfumo wa ufuatiliaji wa video wa serikali umesema barabara kuu hiyo ilifungwa pande zote mbili huku kazi ya uokoaji na uchunguzi ikiendelea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma