

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China akutana na Waziri Mkuu wa Ureno Montenegro
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Ureno Luis Montenegro kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Waziri Mkuu wa Ureno Luis Montenegro mjini Beijing jana Jumanne akisema kwamba China na Ureno ni mataifa yenye historia ndefu na utamaduni tajiri, na watu wa nchi hizo mbili wote wana sifa maalumu ya kufuata ufunguaji mlango, jumuishi, na kusonga mbele kwa kujiendeleza. Ameongeza kuwa pande hizo mbili zimetatua kwa mwafaka suala la Macao kupitia mashauriano ya kirafiki.
Rais Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimepata matunda mengi katika ushirikiano kwenye sekta mbalimbali, zikiweka mfano wa kuheshimiana na kunufaishana kwa nchi zenye mifumo tofauti ya jamii na hali tofauti ya nchi.
Akisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ureno, Rais Xi amesema China inapenda kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na Ureno, kuelekeza uhusiano wa pande mbili kwenye mwelekeo sahihi, kuufanya uhusiano huo mzuri kuwa bora zaidi, na kuchangia zaidi kwenye ustawi na maendeleo ya nchi hizo mbili na dunia kupitia mshikamano na ushirikiano.
Rais Xi ametoa wito kwa pande hizo mbili kuenzi urafiki wa jadi, kudumisha hali ya kuaminiana na kuungana mkono, kuongeza kwa kina uratibu wa mikakati ya maendeleo, na kupanua ushirikiano wa kivitendo katika maeneo kama vile uvumbuzi, maendeleo ya kijani, mambo ya bahari na huduma za afya.
Huku akisema kuwa mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, pamoja na maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN), Rais Xi amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana kwa karibu na Ureno katika mambo ya pande nyingi ili kwa pamoja kutekeleza kweli ushirikiano wa pande nyingi, kulinda mamlaka ya UN na mfumo wa biashara huria, na kuhimiza ujenzi wa mfumo wa usimamizi wa dunia ulio wa haki na usawa zaidi.
Kwa upande wake Montenegro amewasilisha salamu za dhati za Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa kwa Rais Xi, akiongeza kuwa uhusiano wenye mwelekeo wa siku za baadaye kati ya Ureno na China una historia ndefu, na nchi hizo mbili zimetatua kwa mwafaka suala la Macao kupitia mashauriano ya kirafiki.
Amesema uzoefu wenye mafanikio mkoani Macao katika miaka 25 iliyopita unadhihirisha vya kutosha serikali ya Ureno ilifanya uamuzi sahihi, Ureno itaendelea kufuata sera ya kuwepo kwa China moja na haitasahau uungaji mkono na msaada wenye thamani uliotolewa na China katika kipindi kigumu zaidi cha uchumi wa Ureno.
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Ureno Luis Montenegro kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Ding Lin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma