Rais Xi atuma pongezi kwa mwenzake Kim juu ya kuadhimisha miaka 77 tangu kuanzishwa kwa DPRK

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 10, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumanne ametuma salamu za pongezi kwa Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Labor cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu ya Korea ambaye pia ni mwenyekiti wa mambo ya kitaifa wa nchi hiyo (WPK), kwa kuadhimisha miaka 77 tangu kuanzishwa kwa nchi ya DPRK.

Katika salamu zake za pongezi , Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kuwa katika miaka hiyo 77 iliyopita, chama cha WPK kimeshikamana na kuongoza watu wa nchi ya DPRK kusonga mbele siku hadi siku na kuhimiza maendeleo ya mambo yote ya kijamaa nchini humo.

"Katika miaka ya hivi karibuni, chini ya uongozi wa chama cha WPK inayoongozwa na Komredi Katibu Mkuu Kim, watu wa DPRK wamejitahidi sana kutimiza malengo na kutekeleza majukumu yaliyowekwa kwenye Mkutano Mkuu wa 8 wa chama cha WPK, na wamepata mafanikio mengi ya kuridhisha," Rais Xi amesema.

Ameelezea imani yake kwamba watu wa nchi ya DPRK watakaribisha Mkutano Mkuu wa 9 wa chama cha WPK kwa ari kubwa na mafanikio bora, na kufungua ukurasa mpya katika kujenga ujamaa wa mtindo wa DPRK.

Rais Xi akisisitiza kuwa China na DPRK ni majirani wa jadi wenye urafiki wanaokaribiana zaidi kwa milima na mito, amesema Chama cha CPC na serikali ya China siku zote vitafuata sera ya mkakati ya kudumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano mzuri kati ya China na DPRK.

Rais Xi amesema kuwa siku chache zilizopita, Rais Kim alikuja China kushiriki kwenye kumbukumbu za kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, alikutana tena na Kim na kwa pamoja kupanga dira ya maendeleo ya uhusiano kati ya vyama viwili na nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema upande wa China unapenda kuimarisha uratibu wa kimkakati, kudumisha mawasiliano na ushirikiano wa karibu na DPRK, na kuungana mkono kuhimiza urafiki kati ya China na DPRK na mambo ya ujamaa ya nchi hizo mbili, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo katika kanda na dunia kwa ujumla. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha