

Lugha Nyingine
Rais wa China atuma salamu za pongezi kwa Maonesho ya CIFTIS
Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China (CIFTIS) Mwaka 2025.
Kwenye salamu zake zilizotumwa leo Jumatano, Rais Xi amebainisha kuwa, siku hizi mazingira ya uchumi duniani yanapitia mabadiliko makubwa, na changamoto na fursa zinatokea sambamba katika maendeleo ya dunia, akisema China itaendelea kudhamiria kithabiti katika kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya biashara ya huduma.
Ameongeza kuwa China iko tayari kufanya kazi na pande zote ili kwa pamoja kuhimiza ushirikiano wazi na wa kivumbuzi zaidi katika biashara ya huduma duniani, kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, na kuingiza nguvu mpya katika ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma