

Lugha Nyingine
Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN wafunguliwa New York
Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) umetangazwa kufunguliwa rasmi jana Jumanne katika makao makuu ya Umoja huo mjini New York na Mwenyekiti mpya wa UNGA Annalena Baerbock.
Kauli mbiu ya mkutano huo wa 80 wa UNGA, ambao unaadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa ni "Bora Pamoja: Miaka 80 na Zaidi kwa Amani, Maendeleo na Haki za Binadamu".
"Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa si mkutano wa kawaida," Baerbock amesema katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye kikao cha wajumbe wote cha Mkutano huo wa 80.
"Miaka 80. Mirefu zaidi kuliko wastani wa umri wa uhai wa binadamu. Kwa kawaida, huu ulipaswa kuwa wakati wa kusherehekea lakini tuko kweli katika hisia za kusherehekea?" Rais huyo mpya wa UNGA ameuliza.
Amesema, wazazi Gaza wanatazama watoto wao wakifa kwa njaa, wasichana wa Afghanistan wanapigwa marufuku kwenda shuleni, wanawake wa Darfur wanaficha mabinti zao ili kuwaepusha kubakwa, wakazi wa visiwa vya Bahari ya Pasifiki wanatazama kiwango cha maji ya bahari kikiongezeka na mawimbi yakizunguka karibu na nyumba zao, na watu zaidi ya milioni 808 bado wamenaswa katika umaskini uliokithiri.
Wiki ya ngazi ya juu ya mkutano huo wa UNGA itaanza tarehe 22 hadi 30 Septemba, ambapo katika kipindi hicho viongozi wa nchi mbalimbali watakusanyika kuhudhuria Mjadala Mkuu na mikutano mfululizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma