

Lugha Nyingine
Zambia yafanya mkutano kukabiliana na changamoto za wachimbaji wadogo wa madini
Mkutano wa kupanga upya sekta ya ufundi stadi na wachimbaji wadogo (ASM) umefunguliwa jana Jumanne katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, huku rais wa nchi hiyo Hakainde Hichilema akirejea tena ahadi ya serikali ya kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanafaidika kutokana na utajiri wa madini wa nchi hiyo.
Mkutano huo uliofanyika chini ya kaulimbiu "Kufungua Fursa za ASM kwa Maendeleo Endelevu na Jumuishi" umekutanisha wadau wengi, wakiwemo wachimbaji, ili kutafuta suluhisho la changamoto zinazojitokeza mara kwa mara.
Rais Hichilema ameeleza wasiwasi wake kuhusu mazingira hatarishi ya uchimbaji ambayo yamesababisha vifo vya watu, na kutoa tahadhari dhidi ya matumizi ya madini ya mercury katika uchakataji wa madini, akisema yanahatarisha rasilimali ya maji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma