

Lugha Nyingine
Uganda yaanza kutoa mafunzo kwa wanajeshi 1,800 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jumla ya wanajeshi 1,800 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) wamewasili Uganda kwa mafunzo ya kijeshi ikiwa ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kujenga uwezo wa jeshi la CAR.
Akiongea kwa njia ya simu na Shirika la habari la China, Xinhua, msemaji wa jeshi la Uganda, Meja Jenerali Felix Kulayigye, amesema wanajeshi hao watapitia mafunzo makali ya kimsingi na mazoezi ya kukusanya taarifa za kijasusi katika kipindi cha miezi tisa hadi 12.
Amesema mpango huo wa mafunzo ni sehemu ya makubaliano ya pande mbili ya mwaka 2024 yenye lengo la kuvipa taaluma vikosi vya kijeshi vya CAR na kuimarisha uwezo wao wa kukabiliana na ukosefu wa usalama, kuhimiza amani na kuimarisha utulivu wa kikanda.
Uganda inadumisha ushirikiano wa kimkakati wa ulinzi na CAR, hasa katika juhudi za kupambana na kundi la waasi wa Uganda la Lord’s Resistance Army (LRA), ambalo limekuwa likiendesha shughuli zake nchini humo kwa muda mrefu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma