Mkutano wa 10 wa Kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja wafunguliwa Hong Kong, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2025

Wageni wakihudhuria mazungumzo  kuhusu sera juu ya Kukumbatia Fursa Zinazoibuka katika  kipindi cha hali ya Sintofahamu Kiuchumi kwenye Mkutano wa 10 wa kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja  huko Hong Kong, kusini mwa China, Septemba 10, 2025. (Xinhua/Chen Duo)

HONG KONG - Mkutano wa 10 wa Kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja umefunguliwa huko Hong Kong jana Jumatano, ukikutanisha maofisa muhimu na viongozi wa biashara kutoka nchi na maeneo ya Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kutafuta fursa mpya za ushirikiano na kujenga mustakabali wenye manufaa kwa pande zote.

John Lee, ofisa mtendaji mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, amesema katika hotuba yake kwamba miaka zaidi ya 10 iliyopita, watu zaidi ya 45,000 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 120 wamehudhuria kwenye mkutano huo.

"Kwa pamoja, wamewasilisha miradi zaidi ya 2,800 kwenye Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kueleza matarajio ya pamoja kwa kupitia ushirikiano na mafungamano " amesema.

Amesema, ikiwa "kiunganishi bora" na "kiongeza thamani bora" kwa ushirikiano wa kiwango cha juu duniani kote, Hong Kong itaendelea kuchochea maendeleo ya sifa bora kwenye Ukanda Mmoja, Njia Moja.

"Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja ni tegemeo la uhai kwa maendeleo yetu ya jamii na uchumi. Limetoa rasilimali na ushirikiano tunaohitaji ili kujenga msingi wa ukuaji," amesema Naibu Waziri Mkuu wa Cambodia Sun Chanthol katika hotuba yake kuu, akiongeza kuwa miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja inahusiana karibu sana na maisha ya watu wa kawaida wa Cambodia kila siku.

Ukiwa ni shughuli ya kimsingi kwa kuunga mkono Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, mkutano huo utasaidia kampuni kupanua biashara na kuwezesha upigaji hatua katika miradi mbalimbali. 

Wageni wakishiriki kwenye  Hafla ya Makabidhiano ya  Makubaliano ya Maelewano (MoU) kwenye Mkutano wa 10 wa kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja  huko Hong Kong, kusini mwa China, Septemba 10, 2025. (Xinhua/Chen Duo)

Mkutano wa 10 wa kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ukifanyika  huko Hong Kong, kusini mwa China, Septemba 10, 2025. (Xinhua/Chen Duo)

Mkutano wa 10 wa kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ukifanyika huko Hong Kong, kusini mwa China, Septemba 10, 2025. (Xinhua/Chen Duo)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha