

Lugha Nyingine
Maeneo manne ya China yaongezwa kwenye orodha ya Miundombinu ya Umwagiliaji ya Urithi wa Dunia
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2025
![]() |
Picha iliyopigwa Septemba 10, 2025 ikionyesha mwonekano wa Mfumo wa Umwagiliaji wa Jianjiangyan ulioko Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China. (Picha na Zhang Yong/Xinhua) |
Maeneo manne ya China yameongezwa kwenye orodha ya Miundombinu ya Umwagiliaji ya Urithi wa Dunia (WHIS), Wizara ya Rasilimali za Maji ya China imetangaza jana Jumatano.
Maeneo hayo manne ya China, ambayo ni Mfumo wa Umwagiliaji wa Ziwa Chishan, Mashamba ya Kwenye Miteremko Milimani ya Kabila la Wahani ya Yuanyang, Mfumo wa Umwagiliaji wa Jianjiangyan, na Mifereji ya Kale ya Mentougou ya Mto Yongding, yamechaguliwa kuungana na kundi jipya la maeneo yaliyoongezwa kwenye orodha hiyo ya WHIS katika Mkutano unaoendelea wa 76 wa Baraza Kuu Tendaji la Kimataifa la Kamisheni ya Kimataifa juu ya Umwagiliaji na Utiririshaji Maji (ICID).
Mkutano huo ulifanyika Kuala Lumpur, Malaysia.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma