China yapenda kushiriki kikamilifu katika kuboresha usimamizi wa haki za binadamu duniani: balozi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2025

Picha hii iliyopigwa Septemba 9, 2025 ikionyesha mkutano wa 60 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva, Uswisi. (Xinhua/Lian Yi)

Picha hii iliyopigwa Septemba 9, 2025 ikionyesha mkutano wa 60 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva, Uswisi. (Xinhua/Lian Yi)

GENEVA - China inapenda kushiriki kikamilifu katika kuboresha usimamizi wa haki za binadamu duniani, Chen Xu, mwakilishi wa kudumu wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswizi amesema Jumanne wakati akihutubia mkutano wa 60 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ambapo pia amefafanua juu ya msimamo na mapendekezo ya China katika usimamizi wa haki za binadamu duniani.

Chen amesema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, na kwamba usimamizi wa dunia bado unakabiliwa na changamoto kubwa.

“Mpango wa usimamizi wa dunia unaopendekezwa na China unalenga kuhimiza utaratibu wa kimataifa kuelekea haki na usawa zaidi,” amesema.

Kuhusu usimamizi wa haki za binadamu, Chen amesisitiza kanuni tatu muhimu:

Kwanza, China inashikilia usawa wa mamlaka na utawala wa sheria za kimataifa.

Amesema pande zote zinapaswa kufuata madhumuni na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, kuheshimu mamlaka ya nchi na haki yao ya kuchagua kwa kujitegemea njia zao za maendeleo ya haki za binadamu, na kupinga kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha haki za binadamu.

"Kwa mfano, China inaunga mkono mambo ya haki ya watu wa Palestina katika kurejesha haki zao halali za kitaifa." amesema.

Pili, China inatetea mfumo wa pande nyingi na ushirikiano thabiti zaidi wa kimataifa.

"Hakuna mfano unaotumika duniani kote kwa maendeleo ya haki za binadamu," Chen amesema, akiongeza kuwa uanuwai wa ustaarabu wa dunia unapaswa kuheshimiwa, na mazungumzo na ushirikiano vinapaswa kupewa kipaumbele.

Tatu, China inatoa wito wa kuwa na mtazamo unaozingatia watu na kuchukua hatua.

Amesema, watu wote ni washiriki na wanufaika wa usimamizi wa dunia na kwamba ni muhimu kusisitiza tena dhamira ya kuanzishwa kwa Baraza la Haki za Binadamu ili kuhimiza na kulinda haki za binadamu, kutoa kipaumbele sawa kwa aina zote za haki, na kusukuma mbele haki kwa uwiano, wakati huo huo kuharakisha kutambuliwa na kufikiwa kwa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni na haki ya maendeleo.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN) Volker Turk akizungumza katika mkutano wa 60 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Lian Yi)

Chen Xu, mwakilishi wa kudumu wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswisi, akihutubia mkutano wa 60 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Lian Yi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha