

Lugha Nyingine
Makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 48 za kimarekani yafikiwa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Ndani ya Afrika
Benki ya Exim ya Afrika (Afreximbank) imesema Maonyesho ya nne ya Biashara ya Ndani ya Afrika (IATF 2025) yaliyofungwa Jumatano mjini Algiers nchini Algeria, yameshuhudia makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 48.2 za kimarekani yakifikiwa.
Mkuu wa Afreximbank Benedict Oramah ameyaelezea matokeo hayo kuwa yenye mafanikio makubwa zaidi tangu maonesho hayo yaanze kufanyika, yakipita makadirio ya awali ya dola bilioni 44.
Amesema, kati ya thamani hiyo ya jumla ya makubaliano hayo, Algeria imechukua makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 11.6 za kimarekani, au karibu ya robo ya thamani ya jumla.
Makubaliano hayo yaliyofikiwa yanahusiana na sekta zikiwemo za kilimo, nishati, mambo ya fedha, afya na uchukuzi.
Maonyesho hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na Afreximbank, Umoja wa Afrika, na Sekretarieti ya Eneo la Biashara Huria Barani Afrika (AfCFTA), yamefanyika kuanzia tarehe 4 hadi 10 Septemba na kuvutia washiriki zaidi ya elfu 35 na waoneshaji bidhaa elfu mbili kutoka nchi zaidi ya 75.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma