

Lugha Nyingine
Maonesho ya utalii yafunguliwa nchini Zimbabwe kuonesha vivutio na kujenga ushirikiano
Maonesho ya kimataifa ya utalii ya Sanganai/Hlanganani/Kumbanayi ya Zimbabwe yamefunguliwa mjini Mutare katika Jimbo la Manicaland, yakilenga kuonesha vivutio vya utalii vya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika na kujenga ushirikiano wa kibiashara.
Maonesho hayo ni ya kila mwaka yakiandaliwa na Wizara ya Utalii na Sekta ya Hoteli ya Zimbabwe kwa ushirikiano na Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe na kwa mwaka huu yanafanyika chini ya kaulimbiu ya "Kugatua Maendeleo Endelevu ya Utalii-Mustakabali Wetu".
Akifungua rasmi maonesho hayo Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema, "Maonesho haya ya utalii ni mahali ambako utamaduni unakutana na biashara, mazingira ya asili yanapokutana na uvumbuzi, na mahali ambapo Zimbabwe inajiweka katika nafasi ya kuwa kivutio cha utalii kinachoongoza."
Amesema, utalii nchini Zimbabwe umehimiza maendeleo ya kampuni za wenyeji, kuwezesha jamii na kuchochea juhudi za uhifadhi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma